Uzinduzi
huu wa viatu vya SULTAN klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel ulibarikiwa
na viongozi wa serikali, wanamzuziki, wanamitindo, wabunifu, waigizaji
na watu wengi mashuhuri.

Mshindiwa
Big brother Afrika 2014 Idris Sultan amezindua viatu vyake viitwavyo
SULTAN by FOREMEN akiwa pamoja na klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel.
Uzinduzi huu ulifanyika pamoja kama namna ya kuwaunganisha wanaume wa
Tanzania kuwa sehemu ya viatu hivi maalum na umoja endelevu.
SULTAN
by FORMEN ni chapa ya viatu iliyotengenezwa kwa kuzingatia unadhifu,
ubora, starehe (comfort) na hadhi ya uzito wa viatu vya mwanaume wa
kitanzania.
“Tumetengeneza
dizaini tofauti zit akazoingia sokoni kubadilisha ulimwengu wa fasheni
katika usafi, unadhifu, furahanauchangamfu. Aina hii ya viatu
inawakilisha mwanaume wa kitanzania anayefanya kazi zake kwa bidii, kwa
ubunifu akiwa na muonekano wa tofauti unaopendeza” asema Idris.
Chapa
hii ya SULTAN by FOREMEN ni mafanikio mapya kwa Idris ukiacha mafanikio
yake mengine aliyoyapata hivi karibuni kama kuchaguliwa kuigiza katika
movie ya Hollywood marekani itakayogharimu takribani dola million 5.
Idris
ambaye alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu Tanzania baada
ya kushiriki katika filamu ya KIUMENI ambayo imeshinda tunzo mbili
katika tamasha la filamu la ZIFF
Idris
ni mchekeshaji na kijana maarufu anayependa kuvaa vizuri na kwenda na
wakati hivyo atauza viatu hivi kwa bei nafuu ilikila mtanzania aweze
kuvimudu.
No comments:
Post a Comment