jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

RAS PWANI AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA UMUHIMU WA KUSHIRIKI UZINDUZI MWENGE WA UHURU

Share This


WhatsApp%20Image%202025-03-28%20at%205.23.55%20PM%20(1)

WhatsApp%20Image%202025-03-28%20at%205.23.56%20PM



Na Khadija Kalili Michuzi TV
KATIBU Tawala Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania Rashidi Mchatta amefungua Kongamano la siku mbili lililojikita katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa uzinduzi na mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Bertil Merlin na kuwakutanisha wanafunzi wa Kibaha Sekondari, Chuo Cha Afya na Sayansi Tumbi.

" Nawashukuru waandaji na washiriki wa Kongamano hili muhimu la vijana kuhusu umuhimu wa kushiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 ambalo litafanyika siku mbili leo tarehe 28 hadi 29 Machi 2025."

"Serikali inatambua umuhimu wa kundi la vijana katika kuleta mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi kutokana na ari, nguvu na ubunifu walionao. Kwa kutambua hilo serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikitoa kipaumbele kwa vijana kupata elimu na makuzi bora, kuwapa fursa ya kupata mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri na Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build Better Tomorrow – BBT) " amesema RAS Mchatta.

Amesema Kongamano hili limeandaliwa katika mtazamo wa kuwajengea uwezo vijana juu ya umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika kujenga udugu, utu, uzalendo, uwajibikaji katika usimamizi wa shughuli za maendeleo na kutambua fursa za kiuchumi.

"Nimeambiwa kuwa mada zitakazojadiliwa kwa siku mbili ni kama zifuatazo:- Historia na Falsafa ya Mwenge wa Uhuru Uzalendo, Itifaki na Maadili

Fursa za Kiuchumi zinazotokana na Mwenge wa Uhuru

Umuhimu wa kushiriki katika shughuli za utunzaji wa nazingira

Umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

stadi za maisha na stadi za kazi

malezi na makuzi kwa vijana

afya na afya ya uzazi

Sambamba na mada hizo itatolewa elimu ya matumizi sahihi ya Mitandao ya simu na elimu ya utunzaji wa fedha katika Taasisi za kifedha.

" Nawasihi vijana kusikiliza kwa makini na kutafakari mada hizo ili ziweze kuleta mabadiliko chanya kimtazamo katika maisha yenu binafsi, kijamii na maendeleo ya nchi yetu" amesema Mchatta.

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 utazinduliwa Mkoa wa Pwani kitendo ambacho kinaonesha nia njema ya dhahiri Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuendeleza na kuenzi kwa vitendo yale yote aliyoturithisha baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage.

Tarehe 2 Aprili 2025 Mbio za Mwenge wa Uhuru zitazinduliwa katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani ambapo mgeni Rasmi atakuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 ni ‘Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka 2025 Kwa Amani na Utulivu'.

"Rai yangu kwenu mjitokeze kushiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa namna ambavyo mtaelekezwa na viongozi katika maeneo mnayoishi" amesema Mchatta.

"Tukifanya hivyo tutaupata ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa ufasaha ili muweze kushuhudia kwa vitendo yale yote mtakayojifunza katika Kongamano hili" amesema Mchatta.

Kongamano hili litahitimishwa t na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.

Wakati huohuo Benki NMB imechangia kiasi cha Mil.30 ili kufanikisha Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru.


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlandizi. William Marwa mesema kuwa Benki ya NMB wamechangia kiasi cha Mil.30 ikiwa ni katika kufanikisha Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru utakaofanyika Aprili 2 ,2025 kwenye Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani ambapo wahudhuriaji 16,000 wanatajiwa kushuhudia uzinduzi huo.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad