Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Bi. Khadija Ngasongwa amewataka watumishi wa FCC kufanya kazi kwa ushirikiano, bidii, upendo pamoja na ubunifu katika utendaji ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Bi. Ngasongwa ametoa wito huo Aprili 9, 2026 wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa FCC uliofanyika Manispaa ya Morogoro.
Amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
"Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku." amesema Bi. Khadija
Ameongeza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro, maslahi ya watumishi na kuboresha mazingira ya kazi. Aidha, amewataka watumishi kuzingatia haki, wajibu pamoja na maadili ya Utumishi wa Umma.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Tughe Taifa Bw. Samwel Nyungwa amesema mabaraza ya wafanyakazi yameendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya uongozi na watumishi huku akiwapongeza FCC kwa juhudi zao katika kuboresha utendaji kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya taasisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
FCC itaendelea kuthamini mchango wa Baraza la Wafanyakazi kama chombo muhimu cha ushirikishwaji katika maamuzi ya kimkakati na uendeshaji wa taasisi, sambamba na azma ya kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma bora kwa jamii.
FCC YAWATAKA WATUMISHI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UBUNIFU KAZINI
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.





















No comments:
Post a Comment