JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SERIKALI YAHIMIZA MAENDELEO YA KIKANDA NA MIPANGO MIJI KUKUZA UCHUMI AFRICA

Share This
Na Munir Shemweta, WANMM NAIROBI


Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuunganisha maendeleo ya kikanda, mipango miji pamoja na miundombinu kama nyenzo muhimu ya kuchochea ukuaji wa uchumi na ujumuishaji wa kikanda Barani Africa.

Akizungumza katika mjadala wa kitaalamu uliofanyika sambamba na Kongamano la Pili la Miji Afrca (2nd Africa Urban Forum) jijini Nairobi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameeleza kuwa, kanda za maendeleo zina mchango mkubwa katika kurahisisha biashara, usafirishaji na kuunganisha nchi zisizo na bandari na masoko ya kimataifa.

‘’Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza kanda mbalimbali tangu miaka ya 1970 ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati’’. amesema

Kwa mujibu wa Dkt Akwilapo, Kanda ya Kati imeendelea kuwa mhimili muhimu wa usafirishaji, ikiunganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia reli, barabara na njia za majini.

Ameongeza kuwa, ongezeko la kasi la ukuaji wa miji limeongeza mahitaji ya miundombinu na huduma, huku mahitaji ya usafiri yakiongezeka mara nne ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita. ‘’Hali hii imeifanya serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya miundombinu na mipango miji ili kukidhi mahitaji hayo’’. ameeleza

Aidha, amesema uwepo Bandari ya Dar es Salaam, Reli za TRC pamoja na ile ya TAZARA umeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha biashara ya kikanda, huku usafiri wa majini katika Maziwa Makuu ukichangia kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi jirani.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameeleza kuwa, Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuboresha miundombinu na makazi, sambamba na kuhimiza ushiriki wa sekta binafsi kupitia ubia na serikali.

Akihitimisha taarifa yake katika mjadala wa kitaaluma, Dkt Akwilapo amezitaka nchi za Africa kuimarisha ushirikiano wa kikanda, mipango miji na miundombinu, akieleza kuwa, hatua hiyo itasaidia kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kuboresha maisha ya wananchi na kupunguza pengo la maendeleo kati ya mijini na vijijini.

Kongamano la pili la Miji Africa limebeba kauli mbiu isemayo “Adequate Housing for All: Advancing Socio-Economic and Environmental Transformation Towards the Realization of Agenda 2063,” ambapo kupitia kongamano hilo kumekuwa na mijadala inayohusisha Mawaziri, Mameya na Wataalamu mbalimbali, lengo likiwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya maendeleo ya miji.



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza katika Mjadala wa Kitaalamu unaofanyika sambamba na Kongamano la Pili la Miji Africa (2nd Africa Urban Forum) jijini Nairobi, Kenya.


Sehemu ya washiriki katika Mjadala wa Kitaalamu uliofanyika sambamba na Kongamano la Pili la Miji Africa (2nd Africa Urban Forum) jijini Nairobi, Kenya ambapo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo alishiriki. ( PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad