Prof.Mkumbo katikati akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa King Lion Arnold Lyimo.
Waziri Mkumbo akiwa kwenye picha ya pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya GFA Assemble
Na Khadija Kalili Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Rais Mipango Na Uwekezaji Prof. Kitila Alexander Mkumbo ametoa ahadi kwa uongozi wa Kiwanda cha King Lion kuwa Serikali itajenga miundombinu rafiki kwa wawekezaji hasa ujenzi wa barabara, kuhakikisha umeme wa uhakika na kuwaunganisha na bomba la gesi .
Waziri Mkumbo amesema hayo tarehe 26 alipotembelea Kiwanda cha King Lion na kuona namna wanavyozalisha bidhaa zao.
"Wawekezaji hawa wamewekeza kiasi cha Bil.150 (Dola za Kimarekani Bil.90) ambapo wanatengeneza mabati meupe na ya mgongo.
"Jambo la kujivunia kuona hivi sasa mabati haya ambayo zamani tulikua tunayaita Msouth yanazalishwa nchini na hiki ndiyo Kiwanda kikubwa barani Afrika na tayari wanauza mabati yao nchi za Rwanda, Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na nchi zingine mbalimbali " amesema Mkumbo.
Mkumbo amesema kuwa anawapongeza King Lion kwa kuzalisha ajira 2,000 huku ajira 800 za moja kwa moja na 1,200 siyo za moja kwa moja.
Aidha Prof. Mkumbo amesema kuwa Serikali inajivunia matunda ya mafunzo ya VETA kutokana na wafanyakazi wengi wa viwandani wamepata mafunzo VETA.
Meneja wa Kiwanda cha King Lion Arnold Lyimo amesema kuwa wanamshkuru Waziri Kitila kwa kufika Kiwandani hapo na kuahidi kutatua changamoto zao kubwa ambazo ni umeme, barabara mbovu pia umuhimu wa kuunganishwa na bomba la asili.
Wakati huohuo Waziri Mkumbo ametembelea Kiwanda cha Kuunga magari kilichopo TAMCO Kibaha na kushuhudia namna magari hayo yanavyoungwa nankuingia sokoni.
Prof.Mkumbo amewapongeza Kampuni ya GFA Assemble na kuwataka waongeze7 uungaji wa GFA magari mengi zaidi.
"Nimeelezwa kuwa GFA walianza kwa kuunga magari 100 na hivi sasa wameongeza idadi ya magari wanaunga magari 3,000" amesema.Prof Mkumbo.
No comments:
Post a Comment