jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO MGENI RASMI UZINDUZI WA MWENGE

Share This

 

WhatsApp%20Image%202025-03-26%20at%202.45.58%20PM%20(1)
Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete (MB)  pichani  leo alipotembelea Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha  Mkoani  Pwani  na kuridhishwa na maandalizi  yaliyofikia kwa asilimia 95

Na Khadija Kalili Michuzi TV
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isidory Mpango atazindua mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 2 Aprili 2025.

Akizungumza leo tarehe 26 Machi 2025 kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwetete (MB) alipozungumza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani.

"Awali ya yoye napenda kutumia fursa hii kumshkuru Mungu kwa kurukutanisha siku ya leo tunapoelekea katika tukio la uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025" amesema Kikwete.

"Napenda kutoa taarifa kwa umma kuwa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru utakuwa katika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani" amesema Kikwete.

Waziri Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani amesema kuwa baada ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 kuzinduliwa Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango atawakabidhi vijana sita waliochaguliwa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, watakaokuwa na jukumu la kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Mikoa 31 yenye jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanza kwa siku 195 na katika kipindi hicho chote,Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja upendo na mshikamano wa Kitaifa .Vilevile Mwenge wa Uhuru utawahimiza wananchi kushiriki.shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao ya Halmashauri.

Kauli mbiu mwaka huu umebeba kaulimbniu isemayo 'Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu 'ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu unalenga kuwaelimisha na kuwaunganishs wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu kwa amani utakaofanyika mwaka huu.

Aidha Mwenge wa Uhuru utatumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini juu ya masuala ya kisekta na katika muktadha wa Kitaifa na Kimataifa ikiwa ni pamoja na maradhi yanayotishia ustawi wa watu kama vile UKIMWI, Malaria na kupambana na matumizi ya Dawa za Kulevya na Vitendo vya rushwa .Vilevile katika Halmashauri zote utakapokuwa Mwenge wa Uhuru utaendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa Lishe Bora kwa afya imara.

Mwaka 1961 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliuwasha Mwenge wa Uhuru na kumkabidhi Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa Luteni Alexander Ngweba Nyirenda na kikosi cha vijana wenzake wakaupandisha Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanganyika juu ya Mlima Kilimanjaro. Mwalimu Nyerere wakati akitoa hotuba ya siku ya Uhuru aliwatangazia Watanganyika , Afrika na Dunia kwa ujumla kwa kutamka maneno haya"Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu,ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini,ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali penye dharau" amesema Mhe.Kikwete.

"Watanzania wenzangu tunatambua kuwa falsafa hii ya Mwenge wa Uhuru, ndiyo chimbuko la Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964,Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964 na Azimio la Arusha la mwaka 1967.Niwasisitize watanza tuendeleze Mwenge wa Uhu kama ulivyo asisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage mwaka 1961 wakati Taifa letu lilipopata Uhuru" amesema.

"Napenda kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Pwani,Mikoa ya jirani na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi"amesema Mhe.Kikwete.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad