JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MABORESHO YA KIMFUMO, KIMUUNDO YA JESHI LA MAGEREZA KUNUFAISHA MAGEREZA YA UZALISHAJI MALI NCHINI

Share This

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza baada ya kufika katika Gereza la Kilimo na Ufugaji Kitai, Mbinga, Mkoani Ruvuma Septemba 29, 2024. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoa Ruvuma katika Gereza la Kilimo na Ufugaji  Kitai, Mbinga, Mkoani Ruvuma Septemba 29, 2024, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makori.

Na. Mwandishi Wetu, MoHA, Septemba 30, 2024
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Jeshi la Magereza lazima likubaliane na maboresho ya kimfumo, kimuundo na kitaasisi ambayo yatakwenda kuongeza uwezo wa uzalishaji mazao ya kilimo kwa magereza ya uzalishaji mali nchini.

Waziri Masauni ameyasema hayo tarehe 29 Septemba, 2024 alipotembelea na kuzungumza na Maafisa wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai, Mbinga Mkoani Ruvuma ambapo amesema miongoni mwa maboresho hayo ni kutenganisha mamlaka ya kiutawala ya Jeshi la Magereza na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo (SHIMA), ambapo maboresho yatakwenda kuleta ufanisi wa usimamizi wa mauasala ya kiutawala na biashara.

Aidha Waziri Masauni katika hatua nyingine ametoa maagizo kwa magereza ya uzalishaji mali nchini nzima kuchangamkia fursa za kilimo cha mazao ya nafaka kwa kutanua maeneo ya mashamba ili kuendana na jitihada za Serikali katika kuinua sekta ya kilimo.

"Serikali imetanua fursa ya soko la mazao ya nafaka kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambayo imepewa uwezo na Serikali kununua mazao kwa bei kubwa lakini mpaka sasa bado hakuna jitihada zilizofanywa na Jeshi la Magereza kuchagamkia fursa hii". Alisema Mhandisi Masauni.

Sambamba na hilo Mhandisi Masauni alisisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuacha na matumizi ya kuni na mkaa katika magereza ili kuendana na ajenda ya Afrika na Dunia katika kutunza mazingira.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai SP. Gabriel Luderi amesema Gereza hilo lipo tayari kupokea na kuendana na mabadiliko yakatayoongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Magereza.

Awali Waziri Masauni alitembelea Gereza hilo mwaka 2019 akiwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo ambapo amesema licha ya kuwa sasa kuna mabadiliko lakini alitarajia kuona mabadiliko makubwa zaidi ya Kilimo katika gereza hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad