JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BUSTANI YA RUVU JKT WAMLETA SIMBA -MEJA KUWASSA

Share This







Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
IMEFAHAMIKA Uongozi wa Bustani ya wanyamapori ya Ruvu 832 JKT iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani watamleta Simba ikiwa ni katika kuiongezea hadhi.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni kwenye bustani hiyo Meja Seif Hassan Kuwassa amesema kuwa bustani hiyo yenye ukubwa wa heka 70 na kujengewa uzio ina wanayamapori aina saba kwa sasa lakini hivi karibuni watamleta Simba ambaye atafunguwa kwenye banda maalumu tofauti na ilivyo wa wanyamapori waliopo hivi sasa ambao wamekua wakitembea kwa uhuru.

Meja Kuwassa anawataja wanyamapori wanaopatikana hivi sasa kwenye bustani hiyo ya 'Ruvu Wildlife' kuwa ni Twiga, Pofu,Pundamilia,Swala aina mbili Impala na Pongo,Nyumbu na ndege wa aina mbili Mbuni asiyeruka na Korongo.

Amesema kuwa wanayama hao ambao ukifika wanaonekana wakiwa wanatembea bila kizuizi wamepatiwa mafunzo ya kuishi na binadamu hivyo hawana madhara.

"Kabla ya kuachiwa kweye bustani wanyamapori hawa wamepatiwa mafunzo na mtaalamu wa wanyamapori ndiyo maana wanaishi kitafiki hata wakiona watu wanafuata bika ya uoga wa aina yeyote, mtalii akifika kuna maelekezo atapatiwa na wataalamu wetu hivyo atakuwa huru kuwalisha chakula maalumu na kupiga nao picha kwa karibu" amesema Meja Kuwassa.

Meja Kuwassa amezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832 Kanali Peter Elius Mnyani, ambaye ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa mradi huo ameongeza kwa kusema kuwa kuna wanyama wengine ambao wanapatiwa mafunzo na baada ya miezi sita watawaachia kwenye bustani hivyo idadi ya wanyama hao itaongezeka na kuleta kivutio zaidi.

"Wazo la kuanzishwa kwa bustani hii limetoka kwa Kanali Mnyani akalifikisha kwenye bodi likapita bila kupingwa na kuzinduliwa mwezi Mei 2024 " amesema Meja Kuwassa.

"Mradi huu una lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan jinsi anavyoitangaza nchi kwa kupitia utalii ndani na nje ya nchi hivyo nasi tumeamua kuutangaza utalii wa ndani amesisitiza Meja Kuwassa.

Amesema kuwa tangu bustani ilipozinduliwa muitikio wake unaridhisha kwani hupata watalii wa nje saba ndani ya juma na mwishoni mwa wiki familia mbalimbali huenda kubarizi katika bustani hiyo.

Amesema kuwa huduma zingine zinazopatikana ni pamoja na kuwa na mabwawa ya kuogelea kwa wakubwa na watoto, kadhalika kuna michezo mbalimbali ya watoto kama kuendesha gari ,baiskeli inapatikana, chakula kinapatikana pamoja na vinywaji aina zote.

Meja Kuwassa ametoa wito kwa wakaazi wa maeneo ya Mlandizi na viunga vya jirani ndani na nje ya Mkoa wa Pwani ambao hawajawahi kwenda mbugani kuona wanyamapori wanakaribishwa 'Ruvu Wildlife' wakajionee wanyama kwa uhalisia kwa sababu panafikika kwa urahisi ni mkabala na barabara ya Morogoro na kuna mandhari nzuri kwa ujumla.

"Huu mradi unajitegemea na tumefuata taratibu zote zinazohusu Wanyamapori" amesema Meja Kuwassa.

Mtaalamu na Mkufunzi wa Wanayapori Ezekiel Mollel amesema kuwa kuna faida ya kwenda mbugani ama bustani ya wanyamapori unaondoa sonona na kuleta afya ya akili.

"Binafsi nina utaalamu wa kongea na wanyama hivyo wakifika hapa wanafungiwa na kupatiwa mafunzo ndani ya miezi sita ndipo wanaachiwa huru kwrnye bustani kama mnavyoona hawana madhara kwa binadamu,wakiona watu wanawafuata kama wanawakaribisha mazingira ya hapa Ruvu ni rafiki kwao wanajiona kama wako mbugani pana rutuba majani yanamea wanakula na hivi vyakula tunavyowapa ni maalumu nikama vitafunywa mbavyo ndivyo watalii wakija tunawapa wawalishe haturuhusu mtu kuingia na chakula au kumpa mnyama kitu chochote cha tofauti" amesema Mollel.

"Kiingilio ni 50,000 kwa mkubwa mtoto 30,000 pia tunazo bei za wanafunzi wa vyuo pia tunaruhusu watu kuja kusherehekea siku zao za kuzaliwa na 'Pre Wedding' kwa ajili ya kupiga picha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad