Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 08, 2023 mara baada ya kutembelea Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
WIZARA ya Maliasili na Utalii wamekuja na teknolojia mpya ambazo zinatumika kwenye uhifadhi wa maliasili, Wanyamapori na Misitu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kutembelea Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa katika sekta ya misitu wamekuwa wakitoa elimu juu ya uhifadhi wa misitu na rasilimali zinazotokana na misitu, mbegu pamoja na kujikita katika kutoa elimu kuhusiana na ufugaji nyuki pamoja na bidhaa zake.
Kuna misitu ya asili pamoja na misitu ya kupandwa ambapo lengo la sekta ya misitu ni kuhakikisha wanaimarisha mifumo ya Ikolojia nchini ili iweze kutoa hewa safi na maji na kuwa na makazi bora ya wanayama pori na kuhakikisha nchi inapata bidhaa bora kutoka katika mazao ya misitu.
Prof. Silayo amesema kuwa TFS imepewa wajibu wa kuhakikisha kwamba nchi inapata bidhaa bora hasa za mazao ya misitu ili iweze kutumika kwenye maendeleo ya taifa kuanzia bidhaa za ujenzi, Nishati zinazotokana na mimea.
Akizungumzia kuhusu sekta ya ufugaji Nyukia Prof. Silayo amesema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi kujihusisha na ufugaji nyuki, Uchakataji wa Mazao ya nyuki, kuboresha mnyororo mzima wa thamani pamoja na usafirishaji katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
"Tumepata masoko makubwa nje ya nchi, Sasa ni wajibu wa wadau wetu wa ndani wanaofanya biashara za kimataifa kuyakaribia masoko hayo na kufanya biashara ya kimataifa pamoja na kuiwezesha nchi kupata fedha za kigeni.
Amesema kuwa ufugaji wa nyuki wanaupa msukumo mkubwa kwani kunamasoko ambayo yameshafanyiwa tathmini za ubora za mazao ya nyuki nchini na zinakidhi vigezo vya uuzaji kwenye masoko ya nje ya nchi.
Amesema TFS wakishirikiana na Serikali wanashirikiana katika upandaji miti ili kuongoa maeneo yaliyoharibika, kuonesha uwekezaji katika maeneo ya viwanda kwamiaka ya hivi karibuni imeweza kuongeza kiwango cha uwekezaji wa ndani na kusafirishaji zaidi mazao ya misitu kuliko ilivyokuwa awali, amesema miaka mitano iliyopita wakuwa qubiki mita (Q³) elfu ishirini na tano kwenda nje ya nchi.
Akizungumzia maonesho hayo Prof. Silayo amewaalika wadau mablimbali kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu juu ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali zinazosimamiwa na TFS.
Amesema kuwa kumekuwa na mageuzi makubwa katika uwekezaji hapa nchini hasa ukiangalia viwanda vilivyowekezwa vimeleta teknolojia ambazo hazikuzoeleka hapo kabla.
Pia amewaasa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa Viwango vya juu ili tusije kuharibu masoko, lakini tuzalishe kwa kiwango kikubwa kwani kwa sasa kiwango ni kidogo
Akizungumzia kuhusiana na uhifadhi wa Misitu amesema kuwa wameweza kutoa mafunzo wa vijana mbalimbali walipo katika maeneo yenye misitu ili waweze kutoa taarifa, kuzuia na kuzima majanga ya moto yanapotokea katika misutu hapa nchini.
Amesema pia serikali imewekeza katika katika teknolojia za kupambana na moto, pia katuma teknolojia ya Satelaiti ambayo inaona moto kabla haujasambaa na kushika kasi na kuweza kutoa taarifa kwa njia za kidijitali ambazo zinasaidia kwenda kuuzima mapema kabla haujaleta madhara.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo akpokea zawadi kutoka kwa mmoja ya wafanyakzi wa TFS Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Juma Mwangi alipotembea katika banda la TFS lililopo kwenye banda la Maliasili na Utalii katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment