Kampuni ya Gf Trucks &
Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imewataka wadau wa sekta ya
Ujenzi ,Wakandarasi , na wadau wa madini pamoja na wafanya biashara
sekta ya usafirishaji nchini kuchangamkia punguzo la bei kwa mashine na
magari (trucks )yanayouzwa na kampuni hiyo ndani ya viwanja vya sabasaba
Akizungumza
na Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina
wakati alipotembelea banda lao ndani ya viwanja vya Maonyesho ya 47 ya
Biashara ya kimataifa.
Afisa masoko Mwandamizi wa kampuni ya GF,
Poul Msuku alisema kampunin ya GF imeamua kuwashika wadau woote katika
sekta ya Madini na Ujenzi kwa kuhakikisha ipo karibu yao kila siku kwa
kutengeneza mpango maalumu utakaowasaidia kupata Mitambo hiyo kwa
Gharama nafuu na kumfikishia mteja hadi nyumban kwake.
Unajua GF
ni wakala wa wauzaji wa mitambo ya XCMG nchini na kuzingatia hilo hivi
sasa XCMG imetimiza miaka 80 ya kutoa sokoni hivyo ni kampuni
iliyokubalika duniani kote katika sekta ya uchimbaji kwani wna mitambo
ya mikubwa na yenye teknolojia ya kisasa hivyo katika kutambua hilo
tumeamua kuwa na offa kwa wteja wetu huku tukisherehekea miaka 80 na
sabasaba kwa pamoja tunajambo kwa wateja.
Poul aliendelea kusema
GF inampango maalumu kwa kushirikiana na Tasisi za kifedha
(mabenki)wameanzisha mpango wa kumkopesha mteja mwenye mradi mitambo kwa
kuzingatia makubaliano maalumu baina ya mteja na beki huku vigezo na
mshariti vikizingatiwa
Mpango huu hasa unawalenga wakandarasi na
wachimbaji wazalendo lengo likiwa ni kuwasaidia kuweza kushindana na
makampuni makubwa ya kigeni
Nae Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa
Madini Tanzania (FEMATA), John Bina aliwataka wachimbaji kuchangamkia
fursa hiyo kwani ni makampuni machache wanaoweza kuwakumbuka na
kuwapatia mitambo kwa staili hiyo apo awali .
FEMATA kupitia
STAMICO waliingia makubaliano na kampuni ya GF Trucks ya kuhakikisha
wanashirikiana katika kuhakikisha wachimbaji wanakwamuliwa kwa kupatiwa
vitendea kazi kwa gharama nafuu,Hivyo aliwapongeza GF na kuwataka
kuendelea kufungua ofisi sehemu zoote zenye migodi ili wwachimbaji
waweze,kiuchangamkia fursa
Mpaka sasa kampuni hiyo imefungua
ofisi katika maeneo mbali mbali nchini ukanda wa kusini yaani mikoa ya
Ruvuma na Mbeya ,kanda ya ziwa wanapatikana Geita na wako mbioni
kufungua ofisi Chunya alimaliza Poul toa punguzo maa lumu kwa wateja
wetu ambao watatembelea banda letu lililopo katika maonyesho ya sabasaba
Akifafanua
zaidi punguzo hilo la bei (sabasaba special) limelenga zaidi katika
mitambo inayotumika kwa shunguli za ujenzi (XCMG Motor grade) ambapo
wakandarasi wazalendo wenye miradi ya ujenzi hii ndio fursa yao kwani
mwaka mpya wa seriklali ndio huu na wakandarasi wazalendo nio
kipamumbele katika hili
Pia wanunuzi na wadau wakubwa wa mitambo
hii ni Makampuni ya Ujenzi,Makandarasi pamoja na wamiliki wa
migodini,Pia tuna magari makubwa ya mizigo FAW,HONG YANG (trucks) pamoja
na tipper zinazotumika katika shunghuli mbalimbali zikiwepo machimbo ya
mchanga na katika baadhi ya halmashauri zimekuwa zikitumiwa kwa
kukusanyia takata na shughuli nyingine.
Akienda mbali zaidi
Lukolo alitanabaisha magari hayo ya FAW na HONG YANG Kwa sasa
yaliotengenezwa na kiwanda cha GFA kinachomilikiwa na watanzania
kilichopo Kibaha mkoani Pwani hivyo katika maonyesho ya mwaka huu
tunajivunia kuonyesha magari yaliotengenezwa na wataalamu wetu
wakishitikiana na wataalamu kutoka nje.
Waziri
mkuu Kassimu majaliwa akiwa ameambatana na Waziri mku mstaafu Mizengo
Pinda wakipita jirani mitambo ya XCMG ndani ya banda la kampuni ya GF
wakati akikagua mabanda katika maonyesho ya biashara ya 47 ya kimataifa
jijini Dar es salaam.
Afisa
mauzo mwandamizi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment's Ltd Poul
Msuku akimwelezea Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania
(FEMATA), John Bina wakati alipotembelea katika maonyesho ya 47 ya
Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam
Pou Msuku akizungumza na wawakilishi wa EXMG kutoka China kuhusu maonyesho namadhimisho ya miaka 80 ya XCMG sokoni
Moja ya mtambo wa kutengenezea barabara motor greda
No comments:
Post a Comment