Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI imetoa onyo kali kwa Watanzania walionza kutumia vibaya uhuru wa kutoa maoni na kupelekea kutoa kauli ambazo zinahatarisha usalama wa nchi, kuvunja sheria za nchi na kulipasua taifa.
Hayo yamesemwa leo Julai 08, 2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun wakati akizungumza na Wananchama cha Mapinduzi (CCM)wa Kata ya Kindondoni Shamba iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa tawi katika kata hiyolililopo Chuo Kikuu Huria. Amesema kauli hizo hazikubaliki na waache kusingizia uhuru wa kutoa maoni.
"Jambo kubwa ambalo dunia inaendelea kutupa heshima Tanzania uamuzi wake wa kuimarisha diplomasia ya uchumi, Demokrasia na uhuru wa watu kutoa maoni yao kama dhamira njema ya Rais Samia." Amesema
Amesema kuwa CCM kimefungua milango ya kupokea mawazo na ushauri kutoka kwa mtu yoyote kwa kuamini kuwa mawazo, maoni, ushauri wa watu ni mhimu kwani nchi hii ni nchi ya watu na ndio dhamira ya serikali ya awamu ya sita.
"Tutataendelea kupokea ushauri, mawazo na maoni lakini isivyo bahati watanzania wezetu wamekuwa wakitaka kuanza kutumia uhuru huo vibaya." Amesema Mhandisi Masauni
Amesema kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria za nchi na sheria za nchi zitabakia kuwa sheria za nchi pia ametoa rai kwa kila mwananchi kuwajibika na kuhakikisha kwamba sheria za nchi zinasimamiwa kwa masirahi ya watu wa nchi hii.
Pia ametoa wito kwa wananchi wote wanaotumia uhuru huo vibaya uliotolewa kwa dhamira njema katika kuvunja sheria za nchi.
Aidha ameliekeza jeshi la polisi na vyombo vya usalama kuhakikisha hawawafumbii macho kikundi chochote kinachopelekea uvunjifu wa sheria za nchi kwa vitendo au kwa kauli.
Akizungumzia kuhusiana na maendeleo ya nchi Mhandisi Masauni amesema... "Tunaamini kabisa kasi ya maendeleo na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika muda mfupi yametokana na dhamira ya dhati, ya mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan na hatua alizochukua kwa kuongeza wawekezaji, Uchumi kuimarika na mahusiano ya kimataifa kuimarika kiasi cha kusaidia kupata fedha nyingi za masharti nafuu kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu."
Aidha amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kudumisha amani ya nchi ili matunda ya kazi nzuri yanayofanywa na serikali yaweze kunufaisha kizazi kilichopo na kizazi kijacho.
Akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa tawi hilo amesema kuwa misingi iliyowekwa na waasisi wa CCM na waasisi wa Nchi ambao ni Hayati Julius Nyerere wa TANU kwa upande wa Tanganyika na Hayati Amani Abed Karume wa ASP upande wa Zanzibar ambapo vyama hivyo vimezaa CCM.
"Tunapozungumzia Muungano, Mshikamano huwezi kutenga na Chama Cha Mapinduzi(CCM)." Ameeleza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) wa kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam leo Julai 08, 2023.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kinondoni Shamba wakiwa kwenye Uzinduzi wa Tawi lililopo Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam leo Julai 08, 2023.
No comments:
Post a Comment