JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KILIO CHA LUMBESA MADILU CHAMFIKIA MBUNGE KAMONGA.

Share This


Na. Damian Kunambi, Njombe.

Wananchi wa kata ya Madilu iliyopo Wilayani Ludewa Mkoani Njombe wamelalamikia vipimo vya viazi wanavyohitaji wanunuzi ambapo wamekuwa wakihitaji ujazo wa Lumbesa kitu ambacho kinawapa hasara wakulima hao.

Wakitoa malalamiko hayo mbele ya Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga mara baada ya kufika katani hapo na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali vya kata hiyo ikiwa ni ziara ya kupita kijiji kwa kijiji katika jimbo hilo iliyolenga kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi.

Fabian Msigwa ni miongoni mwa wananchi hao amesema japo kilimo cha mwaka huu wamekifanya kwa urahisi kutokana na kupata mbolea za ruzuku kutoka serikalini lakini wanapokuja kuuza mazao hayo wanakumbana na changamoto hiyo inayopelekea waone uraisi walio upata wa mbolea ya ruzuku ni sawa na bure.

"Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupa ruzuku ya mbolea ambayo imetufanya tulime kwa urahisi sana, ila Mbunge wetu tunaomba ufikishe salamu hizi za lumbesa zinatuumiza wakulima na kutufanya tuone kama ruzuku ya mbolea inajifidia kwenye vipimo vya lumbesa ya viazi". Amesema Msigwa.

Aidha kwa upande wake Mbunge Joseph Kamonga amesema agenda hiyo ya lumbesa wataipeleka bungeni kwa kushirikiana na wabunge wenzie wa majimbo ya mkoa wa Njombe lakini pia wataungana na wabunge wa mkoa wa Mbeya ambapo watamuomba waziri wa kilimo Hussein Bashe kuweka mfumo usio umiza wakulima ikiwezekana viazi hivyo kupimwa kwa kilo.

" Wakati wa bunge la akina Makweta na Mathias wale walikuwa na utarabu wa kuungana na kusukuma agenda kwa pamoja hivyo hii hoja ya lumbesa mtanisikia bungeni nikiisemea kwani haiwezekani wakulima mshindwe kunufaika na mazao yenu waje wanufaike watu wengine" Amesema Kamonga.


 





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad