JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BILIONI 18.77 ZIMETUMWA KWENYE AKAUNTI ZA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI HAPA NCHINI.

Share This
 Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Fedha zilizo pelekwa katika halmashauri zote hapa nchini kiasi cha shilingi bilioni 18.77  kwenye akaunti za shule za msingi na Sekondari kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa wanafuzi wa shule zote hapa nchini.
 Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Benno Ndulu akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mpango, Servacius Likwelile.
 Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mpango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3  kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mpango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mpango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo  katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad