JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMPENI YA UWEKAJI AKIBA FNB YAFIKIA TAMATI.

Share This
 Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank Tanzania, Francois Botha akimkabidhi Peter Kimune, mkazi wa Dar es salaam hundi ya shilingi milioni tano baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya benki hiyo kuhamaisisha uwekaji akiba ambayo imefikia tamati. Makabidhiano haya yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachanga (kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Peter Kimune (katikati) mshindi wa kampeni ya uhamasishaji kuweka akiba iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo kwa muda wa miezi mitatu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za reja reja wa benki hiyo Francois Botha. 

(Picha Mpiga Picha Yetu) 

KAMPENI ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba zaidi iliyokuwa ikiendeshwa na First National Bank Tanzania kwa miezi miatu imefika mwisho huku mshindi wa tatu na wa mwisho akikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni tano.

 Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo na kumkabidhi zawadi Peter Kimune, mkazi wa Dar es salaam aliyeibuka mshindi wa mwezi Disemba 2015, Mkuu wa kitengo cha rejareja cha benki hiyo, Francois Botha alisema “imekuwa kampeni ya yenye mafanikio makubwa na ni furaha kuona wateja wengi wakijitokeza kushiriki.” “Kampeni hii haikuwa tu shindano bali pia imetoa somo na kuhamasisha Watanzania wengi kujitokeza kwenye kuweka akiba. FNB inaamini kwamba kupitia kampeni hii imeweza kuhamasisha Watanzania kuweka akiba kwa ajili ya mustakabali salama wa kifedha hapo badae. 

Akiba inaleta uwezo wa kuwekeza siku zijazo na husaidia wakati wa dharula au pale unapotaka kutimiza mipango yako,” alisema Botha. Kampeni hiyo ya uwekaji akiba ilizinduliwa Oktoba, 2015 na kwa miezi mitatu imeweza kutoa nafasi kwa wateja wapya na wa zamani kuingia moja kwa moja kwenye droo kutokana na kila shilingi elfu hamsini waliyoweka kwenye akaunti zao.

 Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni tano, mshindi huyo aliishukuru benki hiyo kwa kuanzisha mpango huo na kuongeza kuwa uwekaji akiba ni muhimu katika uhifadhi wa fedha binafsi na pia husaidia katika kujenga jamii imara yenye uhakika wa kuishi maisha bora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad