JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


AFYA YA ASKOFU KARDINALI PENGO YAZIDI KUIMARIKA.

Share This
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Muhimbili mara baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenad Abdallah leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenad Abdallah, Kulia ni Katibu wa Wizara hiyo, Dk.Mpoki Ulisubisya.
WAZIRI wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu, akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo, katika taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo,  Dk.Mpoki Ulisubisya na katikati ni  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dk. Godwin  Godfrey.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Jenad Abdallah amesema kuwa afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo inaendelea vizuri tofauti na hali aliyokwenda nayo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Januari Mosi akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Profesa Jenad Abdallah amesema kuwa kutokana na huduma anayoipata katika taasisi hiyo, Kardinali Pengo hali yake inaimarika na si muda mrefu anaweza kuruhusiwa.

Profesa Abdallah amesema hata kiongozi huyo akitaka kwenda nje kwa matibabu wataka kujiridhisha na huduma wanayoitoa.

Waziri wa Afya Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemtembelea Muadhama Polycap Kardinali Pengo na kujioanea hali yake na kudai kuwa kiongozi huyo amemkuta akiwa amekaa na tofauti na baadhi mitandao ya Jamii si Globu ya Jamii ya Michuzi zikidai kuwa yuko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Amesema huduma anayoipata Kardinali Pengo atakuwa Balozi mzuri wa kuelezea huduma ya taasisi ya moya ya Jakaya Kikwete na kuwataka watu wengine kwenda kupata huduma hiyo na sio kwenda nje.

Amesema Serikali itaendalea kuboresha huduma hiyo kwa sasa kwa viwango vya dunia Tanzania imefikia asilimia nne na kiwango cha kimataifa cha juu ni asilimia sita.

Wakati huu Waziri huyo amekutana na menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili kusikia changamoto zinazowakabili pamoja na mafanikio walioyapata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad