Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy,
Bi. Warda Kimaro akizungumza katika uzinduzi wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja
Mkuu wa kampuni ya Vuvuzela Bw. Evans
Bukuku
Meneja
Mkuu wa kampuni ya Vuvuzela, Bw. Evans
Bukuku akizungumza jinsi shindano hilo litakavyofanyika katika manispaa 3 za Dar es Salaam uzinduzi huo uliofanyika wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Na kulia ni Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy,
Bi. Warda Kimaro
Wawakilishi
kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) wakiongezea kuhusiana na Valeur Comedy Nights’ wakiwa na
Mkuu wa kampuni ya Vuvuzela Bw. Evans
Bukuku.
TANZANIA Distilleries Limited (TDL) kupitia
chapa yake ya ‘Valeur Superior Brandy’,
kwa kushirikiana na kampuni ya Vuvuzela Company
Ltd leo hii imezindua rasmi shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’.
Hili ni shindano la kusaka, kuinua na kuendeleza vipaji vya Sanaa ya ucheshi
litakaloanza wiki hii jijini Dar Es Salaam.
Vuvuzela ni kampuni inayojihusisha
na Sanaa ya ucheshi, ikimiliki pia onyesho kubwa la Sanaa ya ucheshi jijini Dar
Es Salaam lijulikanalo kama ‘Evans
Comedy Night’.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy,
Bi. Warda Kimaro alisema. “Kauli mbiu ya chapa yetu ya Valeur Superior
Brandy ni ‘Kwa story zinazonoga’.
Watumiaji wapenzi wa Valeur hupenda sana story nzuri wakiwa katika mapumziko
yao, tunaamini kwamba story nzuri na sanaa ya ucheshi vitaweza kufanya
mapumziko ya wapenzi wa Valeur kuwa bora zaidi.
Tumeungana na Vuvuzela
Entertainment na tuko hapa leo kuzindua ‘Valeur Comedy Nights’. Lengo letu
ni kusaka na kukuza vipaji vya Sanaa ya ucheshi hapa Tanzania, kuwafanya
wasanii hawa kugundua fursa waliyo nayo kupitia sanaa hii ya ucheshi.
Bi.
Warda aliendelea kusema kwamba ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika
katika jiji la Dar Es Salaam pekee kwa sasa, lakini ina mpango wa kufika pia
mikoani endapo mambo yakienda vizuri katika msimu huu wa kwanza.
Alisema
washindi 5 watakaofaulu zaidi watapata nafasi ya kujiendeleza Zaidi katika
kampuni ya Vuvuzela Entertainment, na mshindi wa jumla atajipatia kitita cha shilingi 2,000,000/= taslimu.
Aliendelea kusema kwamba wataalamu wa Vuvuzela Company Ltd ndio watahusika
katika kuchuja vipaji na kusimamia shindano kwa ujumla. Bi Warda alisema pia
kwamba wataalika wataalamu wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ili kusimamia
mchuano uwe wa haki kwa washiriki wote.
Naye Meneja
Mkuu wa kampuni ya Vuvuzela Bw. Evans
Bukuku alisema ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika kwa wiki 10 jijini Dar,
ambapo kwa wiki 9 watakuwa wanasaka vipaji wilaya hadi wilaya na wiki ya kumi
ni ya fainali ya mkoa kupata mshindi wa jumla.
Aliendelea kusema usajili
utafanyika siku za Alhamisi ambapo washindi 5 waliofanya vizuri watachuana
katika fainali za wilaya zitakazofanyika Jumamosi hiyo. Mshindi mmoja katika kila
fainali ya wilaya atapata nafasi ya kuingia katika kinyang’anyiro cha fainali
za mkoa ambapo mshindi wa jumla atajipatia fedha taslimu. Bw. Evans alisisitiza
kwamba kampuni yake itachukua wasanii 5 waliofanya vizuri zaidi kwa ajili ya
kuwalea na kuwapa mafunzo zaidi waweze kufika mbali katika fani hii.
Bw. Evans alitaja masharti ya shindano hili
kuwa ni kwa walio na umri wa miaka 18 na zaidi pekee, washiriki hawatakiwi
kutoa utani juu ya mambo ya dini na siasa kwani haya hugusa hisia za watu,
hawaruhusiwi kulewa wakati wa shindano nk. Alitaja pia vigezo vya ushindi
kwamba ni uwezo wa kuwasilisha ujumbe katika namna ya ucheshi zaidi, uwezo wa
kumiliki jukwaa vizuri, uwezo wa kuwasiliana na hadhira mbele yako nk.
Naye mwakilishi
kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) aliipongeza sana kampuni ya TDL kupitia
chapa yake ya Valeur Superior Brandy kwa kujitokeza kusaidia Sanaa hii ya
ucheshi hapa Tanzania.
Aliendelea kusema katika ulimwengu wa sasa Sanaa ya
ucheshi inaweza kumfanya mtu aishi maisha mazuri sana, alitoa mifano ya
mmarekani Kevin Hart na Mnigeria Basketmouth ambao wanafanya vizuri sana sasa
hivi katika Sanaa hii ya ucheshi.
Alisema pia kwamba Sanaa ya ucheshi ni mpya
kwa Tanzania lakini inaonyesha kukua zaidi siku za usoni na kusaidia wasanii wa
Tanzania.
Aliomba makampuni mengine yajitokeze kusaidia maeneo mbalimbali ya
Sanaa ili kuwafanya vijana wengi zaidi kupata ajira katika Sanaa, pia kuwapa
vijana wa Tanzania shughuli za kufanya ili wasikae vijiweni kwenye madawa ya
kulevya na matatizo mengi ya dunia ya sasa.
Naye Meneja
wa mauzo wa kampuni ya TDL kanda ya Dar es Salaam, Bw. Mwesige Mchuruza
alielezea kwamba mashindano haya yatafanyika katika baa mbalimbali jijini Dar
Es Salaam. Kwa wiki hii yakuanzia usajili utafanyika siku ya Alhamisi tar 27
July katika baa ya TCC Club Chang’ombe, na Fainali za wilaya zitafanyika siku
ya Jumamosi tar 01 August katika baa hiyo hiyo na ratiba nyingine ikiwa
ifutavyo;
WEEK
|
AUDITION OUTLET
|
FINAL OUTLET
|
LOCATION
|
1
|
TCC Club
|
TCC Club -
Chang'ombe
|
Chang'ombe
|
2
|
Dar West Park
|
K.B Paradise -
Tabata
|
Tabata
|
3
|
Vijana Social
|
Katumba Bar -
Mkwajuni
|
Kinondoni
|
4
|
Kisuma Bar
|
Kisuma Bar - Mbagala
|
Mbagala
|
5
|
UEFA Bar
|
Mama Land - Ukonga
|
Ukonga
|
6
|
Soccer City
|
Mawella Bar - Sinza
|
Sinza
|
7
|
Brazil Pub
|
Brazil Pub - Tegeta
|
Tegeta
|
8
|
Europa Bar
|
Junction 98 -
Buguruni
|
Buguruni
|
9
|
Blue Fish
|
Liquid Bar -
Kigamboni
|
Kigamboni
|
Bi Warda alimaliza kwa kuwaalika wasanii
wote wa tasnia hii ya ucheshi kujitokeza kwa wingi kuja kujisajili na kushiriki
shindano hili kwani yaweza kuwa mlango wao kuelekea mafanikio makubwa ya
kisanii. Aliwaalika pia wananchi wapenzi wa Valeur Superior Brand kuja kuburudika
na kujionea shindano hili Jumamosi katika baa ya Tcc Club Chang’ombe jijini Dar
Es Salaam. Hakuna kiingilio lakini wanaoruhusiwa ni wale tu wenye umri wa miaka
18 na zaidi.
Wadau wa Valeur Comedy Nights na Valeur Superior Brandy.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Vuvuzela, Bw. Evans Bukuku akipokea hundi ya shilingi mbili kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimar leo.
Baadhi ya vijana wa kampuni ya Vuvuzela wanao weza kuchekesha katika kikundi cha Comedi cha kampuni hiyo.
Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment