Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kueleza uamuzi wa Serikali kuongeza muda wa Sensa ya Viwanda Tanzania Bara hadi Agosti 31,2015 na hatua zitakazochukuliwa kwa viwanda vitakavyoshindwa kutoa takwimu za uzalishaji kwenye Madodoso ya Sensa.
Kaimu Meneja wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkoa wa Dar es salaam Bw.
Albert Kapala akitoa ufafanuzi wa lengo la Sensa ya Viwanda na Idadi ya viwanda
vilivyotoa taarifa za Sensa hiyo jijini Dar es salaam.
NA: Veronica Kazimoto
SERIKALI imeongeza muda wa mwisho wa kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za Sensa
ya viwanda kote nchini hadi Agosti 31 , 2015 kufuatia viwanda vipatavyo 366
vilivyoko jijini Dar es salaam kushindwa kuwasilisha taarifa muhimu za
uzalishaji kwenye madodoso ya Sensa hiyo.
Akitoa
taarifa ya kuongezwa kwa muda wa Sensa hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa Viwanda 366 ambayo ni sawa
na asilimia 20 katika jijini Dar es salaam vimeshindwa kukamilisha na kurudisha
madodoso ya taarifa muhimu za viwanda hivyo.
Amesema
Sensa hiyo ilianza Machi 9 mwaka huu na ilitarajiwa kukamilika Juni 8, 2015
lengo likiwa kukusanya takwimu sahihi zinazohusu Sekta ya Viwanda na mchango
wake katika uchumi wa Tanzania.
Amesema
Sensa hiyo pamoja na mambo mengine ililenga kupata viashiria sahihi vya uchumi
pamoja na taarifa muhimu za viwanda zikiwemo orodha ya viwanda kimkoa, anuani
na mahali vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa wamiliki.
Takwimu
nyingine ni mwaka ambao viwanda hivyo vilianza uzalishaji, shughuli kuu ya
viwanda husika,idadi ya wafanyakazi waliopo,gharama za malipo mbalimbali kwa
wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaj na gharama za uzalishaji.
Ameeleza
kuwa mwaka 2013 Serikali iliamua kuwa ifanyike Sensa ya viwanda nchi nzima ili
kubaini viashiria vya uchumi vitakavyosaidia kuweka mabadiliko ya muundo wa
sekta ya viwanda na mchango wake katika pato la Taifa, kuboresha Sera na
Programu za kukuza ajira, utekelezaji wa Malengo ya Milenia ,Dira ya Maendeleo
ya Tanzania 2025, MKUKUTA na Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Aidha,
ameeleza kuwa jijini Dar es salaam kazi nzuri imefanyika kwa wenye viwanda
kutoa ushirikiano kwa kukamilisha ujazaji wa madodoso mafupi na marefu na
tayari madodoso hayo yameshawasilishwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa uchambuzi.
Mhe.
Saidi
Meck Sadiki amefafanua kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana
na
Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kuhakikisha kuwa asilimia 8
iliyobaki ya viwanda vyote nchini inawasilisha taarifa husika kabla ya
muda uliopangwa.
Amesisitiza
kuwa zoezi hilo liko kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2012 na
watakaoshindwa kutekeleza ujazaji wa madodoso hayo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
"Zoezi
hili ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu linatupa picha ya sekta
ya viwanda nchini pamoja na kuongeza uwazi katika mchango wa sekta ya viwanda
katika Pato la Taifa, hili lazima tulisimamie, wenye viwanda lazima watii
sheria" Amesema.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoa wa Dar
es salaam Albert Kapala amesema kuwa Zoezi hilo ni la kitaifa hivyo taarifa
zote zinazokusanywa ni siri na zinatumika kwa matumizi ya kitakwimu tu.
Amesema
katika Sensa hiyo iliyoanza mwezi Machi mwaka huu mkoa wa Dar es salaam
ulitarajia kuwa umekusanya takwimu za viwanda 1840 ifikapo Juni 8 mwaka huu.
Ameeleza
kuwa hadi sasa viwanda vilivyoshindwa kuwasilisha taarifa kwa mujibu wa Sensa
hiyo jijini Dar es salaam ni 366 wakati vilivyowasilisha ni 1474.
No comments:
Post a Comment