Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea
mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama
kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo,
mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema
litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba
taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia
elimu.
Kauli
hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati
akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa
mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Kongamano
hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye
lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi
na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi
huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa
ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa
kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora
na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu
ambavyo vitaingizwa.
Mratibu
wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa
wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
Yusuph
aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa
kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa
Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya
Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na
kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
Alisema
UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi
ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo
endelevu.
“Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na
waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu
vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
Alisema
kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia
zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha
majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo
ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency
Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo
lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Naye
Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema
kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara
katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha
mafunzo na ufundishaji.
“Leo
tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document
(kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu
watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
Alifafanua
kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na
kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja
mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha
kuridhiwa kwa matumizi.
Naye
kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa
Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya
kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu
huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi.
Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.
Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.
Alisema mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.
Profesa
Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni
matarajio yao kwamba wakishafikisha hati hiyo kwa wizara masuala ya
matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
Pichani
juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano
likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
No comments:
Post a Comment