JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Mhitimu wa VETA Darasa la Tatu B Aanzisha Kiwanda

Share This

 

Mhitimu wa VETA Fani ya Uchomeleaji Faraja Michael akiwa katika bembea aliyobuni ambayo ina sehemu ya kuchaji Simu pamoja sehemu ya maji kwenye Maonesho ya Sabasaba

*Asema ajira za ujuzi zipo za kutosha

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Mhitimu wa VETA Dodoma fani ya uchomeleaji Faraja Michael aanzisha kiwanda chake kutengeneza vitu mbalimbali vinavyotokana na chuma pamoja na Aluminium.

Akizungumza katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya Biashara Kimataifa yanaendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ,Michael amesema kuwa katika maisha na elimu yake ya Darasa la Tatu tu hakuwahi kufikiria kuja kuwa na kiwanda lakini kutokana na mradi E4DT ameweza kuanzisha kiwanda uchomeleaji kwa Ubunifu wa vitu mbalimbali.

Amesema kuwa ujuzi alioupata sasa anaendesha maisha yake na kuondokana na tatizo la ajira.

"VETA imeweza kuniinua kama kijana kupata ajira yangu ya kudumu inayotokana na ujuzi licha ya kuwa darasa la tatu B"amesema Michael.

Michael amesema kuwa kazi kubwa katika ujuzi ni kujituma na kuangalia kitu cha ziada ambacho jamii inahitaji lakini hawezi kupata.

Aidha amesema kuwa vijana wengi wanasema hakuna ajira wakati wakisoma VETA ajira hizo watapata kupitia ujuzi wao.

Hata hivyo amesema VETA ina fani zote ambazo kijana yeyote anaweza kuzifikia lakini kwa kuweka nia yake anataka kuwa nani katika aliosomea.


Amesema kuwa suala la ajira nchini zipo za kutosha changamoto ajira ambazo wanazotaka za kukaa ofisini huku wakisahau ujuzi nao ni ajira

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad