JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BUNGE LAIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI KUVUMBUA BOMU LA KUFUKUZA TEMBO, DORIA ZAANZA WILAYA 24

Share This


Na John Mapepele

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ubunifu wa kuvumbua bomu baridi lililoboreshwa kwa ajili ya kupambana wanyama hatari kama Tembo kwa kushirikiana na Shirika la Mzinga.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava wakati wa hafla maalum ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya kupokea mabomu 4000 yaliyotengenezwa na Shirika la Mzinga mjini Morogoro.

Mara baada ya kupokea mabomu hayo Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza operesheni maalum katika Halmashauri 20 nchini na inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu CP Benedict Wakulyamba.

"Naomba kutoa pongezi za dhati kwa Wizara na Shirika kwa kuja na suluhisho hili na natoa wito kwa halmashauri zinazosumbuliwa na Tembo kununua na kutumia mabomu haya ili kupambana na wanyama hao." amesisitiza Mhe. Mnzava.

Ameitaka Wizara kuendelea kutoa mafunzo kwa askari wa vijiji na vijana kwa kuwa Serikali peke yake haitaweza.

"Hii ni kazi ya sisi sote, Serikali peke yake haitaweza ni lazima kuendelea kuwashirikisha wananchi kwa kuwapa elimu" ameongeza.

Pia ameiomba Wizara kuendelea kufanya tafiti ili kubuni mbinu nzuri zaidi za kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuzingatia kuwa Tembo wamekuwa wakizoea mbinu na kuendelea kuleta usumbufu.

Mwakilishi wa wabunge kutoka kwenye majimbo yenye changamoto za Tembo walioshiriki hafla hiyo, Mhe. Salma Kikwete amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara kwa kuendelea kutatua changamoto hiyo.

"Leo klla Mbunge amefurahi kwa kuwa hili ni jambo kubwa ambalo litaleta suluhisho na sasa tunakwenda kurudisha salamu kwa wananchi wetu kazi hii nzuri iliyofanywa na wananchi" amesisitiza huku akitaka elimu iendelee kutolewa.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki amesema wizara yake itaendelea kutekeleza kikamilifu maelekezo ya viongozi wakuu na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.

Aidha, amesema uvumbuzi wa bomu hilo baridi ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia aliyoitaka wizara kuja na ufumbuzi wa changamoto hiyo.

Ameeleza kuwa wizara yake itaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwa kuwa hakuna njia moja pekee ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Ametumia jukwaa hilo pia kutoa pole kwa wananchi wote ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine.

Hafla hiyo pia iliwashirikisha wabunge, Naibu Katibu Mkuu C.P Benedict Wakulyamba, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ulinzi na menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad