WAOMBAJI wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuwa, baada ya uchambuzi wa maombi yao, Orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupangiwa mikopo imekamilika.
hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru wakati
akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Saaam leo amesema kuwa
Kiasi cha Tshs 34.6 bilioni kimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196. Kwa ujumla, Tshs 108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Amesema kuwa "Orodha hiyo ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika. Orodha nyingine (batches) zitafuata kadri taratibu za udahili na uchambuzi zinavyokamilika.
Lengo ni kutoa majina ya wote waliofanikiwa kupata mkopo kabla ya vyuo
kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba, 2017."
Amesema kuwa Orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua Awamu ya Kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495waliopata udahili katika chuo kimoja.
Wanafunzi
waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wana sifa za
kupata mikopo, watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kuthibitisha chuo
watakachojiunga kwa ajili ya masomo.
Tshs 318 bilioni zatengwa kwa ajili ya wanaoendelea na masomo.
Kiasi cha Tshs 318.6 bilioni kitatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea
na masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Tayari Serikali imeshatoa
fedha hizo na lengo la Bodi ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kabla
ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondoloea wanafunzi usumbufu.
Bodi
ya Mikopo inawasihi waombaji wa mikopo kuwa na subira wakati ikiendelea
kukamilisha maandalizi ya orodha zinazofuata za wanafunzi waliopata
mikopo. Tutaendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na tovuti ya
Bodi mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment