JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LANG’ARA TENA TUZO ZA UBORA DUNIANI.

Share This
Makamu wa Rais wa ShirIka la Ndege la Etihad, Kitengo cha Huduma kwa Wateja Linda Celestino na Meneja Masoko na Mawasiliano Abdulrahman Al-Hadhrami, wakipokea tuzo za  ‘World's Leading Airline’ na ‘World's Leading Airline - First Class’ wakati wa sherehe za 23 za utoaji tuzo hizo zilizofanyika Maldives.

Shirika  la Ndege  la Etihad kwa mara nyingine limenyakua tuzo ya watoa huduma bora wa kwanza zilizotolewa kwa mara ya 23 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) katika sherehe zilizofanyika mwaka huu.

Ushindi huo umelifanya Shirika hilo kufikisha tuzo nane kwa mwaka huu ambazo limezipata kutoka kwa taasisi zinazoheshimika ulimwenguni. Sherehe za kukabidhiwa tuzo hizo zilifanyika kwenye ufukwe wa Sun Siyam Iru Fushi katika visiwa vya Maldives.

Shirika hili la ndege la Etihad pia lilipokea tuzo ya  kuwa watoa huduma bora kwa daraja la kwanza na ukarimu unaotolewa kwa kiwango cha hali ya juu ikiwa ni pamoja na kupigiwa kura kutokana na kuwa na machapisho bora, ushauri na huduma bora zaidi kwa wateja. Tuzo za The World Travel zinajumuisha idadi kubwa ya wapiga kura waliopo katika sekta ya usafirishaji pamoja na watu wengine kutoka kwenye jamii wapatoa  wapigakura 1.2 kwenye Grand Tour 2016.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad alisema, “Dhamira yetu ni kuandaa sera na kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafirishaji wa anga ili iendelee kutambuliwa na kupata tuzo kila mwaka. Tunajivunia kwa mara nyingine tena kwa kupata tuzo hizi mbili za heshima kwa kile tunachoamini kuwa watoa huduma bora na wenye uzoefu kwenye sekta ya usafiri wa anga”

Tuzo za Wold Travel ni jambo la msingi ambapo imewezesha kuonyesha mafanikio ya shirika letu la ndege la Etihad  na kuleta mabadiliko Abu Dhab ambako ndio makao makuu ya shirika hili na kuufanya mji huo kuwa kitovu cha kibiashara na utamaduni ulimwenguni kote.

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa shirika hili la ndege kupokea tuzo mbalimbali za ubora na huduma. Ndani ya mwaka huu tuzo kadhaa zimenyakuliwa zikiwamo ubora wa daraja la kwanza, na nyingine ya hivi karibuni ya utoaji hudma bora Mashariki ya Kati  na huduma bora za mapumziko kwenye uwanja wa ndege katika ukanda huo.

Rais wa Tuzo za Wold Travel, Graham Cooke alisema, “Kwa mara nyingine tena shirika la ndege la etihad limekuwa kinara kwenye sekta ya usafiri wa anga . Wapigakura wa tuzo za Worl Travel hujumuisha wadau waliopo kwenye sekta ya anga pamoja na umma wa watu wengine, ambao ambao wametambua mchango wa shirika hili kwenye usafiri wa anga na kujizolea tuzo. Bila shaka shilika hili lilistahili kupokea heshima hii.”

“Salamu zangu za pongezi nazielekeza kwa timu ya wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Etihad kwa kupata mafanikio haya makubwa na ninatumaini huu ni mwanzo wa kujiandaa na Grand Tour 2017,” Alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad