JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LA SHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA MAFANIKIO YAKE TANZANIA.

Share This

Grace Kijo, Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad nchiniTanzania akigawa chokoleti kwa abiria siku ambayo Shirika hilo liliadhimisha mwaka wake wa kwanza wa huduma zake hapa nchini

Shirika la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake nchi za falme za kiarabu, limetimiza mwaka mmoja wa mafanikio tangu lianze kufanya huduma zake nchini Tanzania ikiwamo kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara ya usafiri wa anga kwa wasafiri wa Dar es Salaam na makao makuu ya falme hizo, Abu Dhabi.

Zaidi ya wasafiri 60,000 wametumia usafiri huo tangu kuzinduliwa kwa huduma zake ambazo zinawaunganisha abiria wengi na miji mikubwa duniani, tangu Desemba Mosi 2015. Wasafiri wengi wamekuwa wakitumia usafiri wa Shirika la ndege la Etihad kutokana na shirika hilo kuwa kitovu cha safari za kwenda Ulaya na Asia.

Shirika hilo linatoa huduma zake kwa kutumia ndege mbili za Airbus A320 yenye nafasi 16 kwa daraja la kwanza na viti 120 kwa daraja la kawaida. Kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam,ndiyo ndege ya tatu kuondoka kutoka Afrika Mashariki ikipitia Uwanja wa Ndege wa Nairobi Kenya na Entebbe Uganda.

Meneja Mkuu wa Kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara wa Shirika la Ndege la Etihad, John Friel alisema, " Kwa mwaka mmoja tangu kuanza kwa huduma zetu kumekuwa na mafanikio makubwa, ndiyo sababu tuliamua kuichagua Tanzania kwa ajuili ya kufanya shughuli zetu. Tunafurahia kufanya kazi kwa ufanisi jambo ambalo limewavutia wateja wengi kulingana na mahitaji ya soko la usafiri wa anga hapa nchini."

"Lengo letu ni kuendelea kushirikiana na wadauwa sekta hii ya anga hapa nchini ili kuhakikisha kwamba abiria wengi zaidi wanatumia usafiri wetu ambao umepata heshima kubwa ulimwenguni kwa kunyakua tuzo mbalimbali za ubora zinazotolewa na Shirika la Ndege la Etihad,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad