JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAPANUA HUDUMA ZAKE ULAYA

Share This
                     Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Shirika la Ndege la Etihad,  imeanzisha ndege tatu kwa ajili ya kuimarisha sekta ya usafirishaji bidhaa barani Ulaya.

Mwezi uliopita kitengo hicho kilianzisha ndege ya boing 777 kutoka East Midlands na Uwanja wa Ndege wa Stansted nchini Uingereza na kutokea Copenhagen nchini Denmark.

Makamu wa Rais, wa Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Etihad, David Kerry alisema, ”Tumetekeleza mahitaji ya wateja wetu kulingana na umuhimu wa usafirishaji nje ya Ulaya, pia ndege zetu zina uwezo wa kutoa huduma kulingana na mazingira yaliyopo pindi inapohitajika.”

Alisema, “Huduma hizi mpya zitawaunganisha wazalishaji na wateja karibu ulimwenguni kote. Wazalishaji nchini Uingereza na Denmark sasa wanaweza kukutana na wateja wao waliopo Mashariki ya Kati kwa haraka zaidi ndani ya masaa 24.”
Mwendeshaji Mkuu wa uwanja wa Copenhagen Airport, Peter Krogsgaard alisema,” Tunayofuraha kwa Kitengo cha Usafirishaji cha Etihad Cargo kuanzisha shughuli zake katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen. Usafirishaji mizigo kwa njia ya anga ni muhimu zaidi kwa ukuaji wa haraka kibiashara kwa Wadenmak. Asilimia kubwa ya Wadenmark hutumia zaidi huduma za usafirishaji kwa njia ya anga ambao pia wengi wao ni ndege.

Copenhagen ni kitovu muhimu cha biashara kwa Ukanda wa Ulaya Kaskazini kwa usafirishaji wa mizigo kwa anjia ya anga na kimataifa kutokana na uwekezaji uliofanywa na shirika la ndege la etihad katika kuimarisha soko la kimaraifa.”

Safari hizi mpya zimewezesha kufikia tisa kwa ndege zinazofanya safari zake Ulaya. Tayari Kitengo cha Usafririshaji cha Etihad kimeifikia miji mingine Ulaya kama vile Amsterdam, Frankfurt (Frankfurt Main na Frankfurt-Hahn), Milan, Brussels pamoja na Zaragoza ikiwamo na huduma za usafiri wa anga kwa abiria katika maeneo mbalimbali barani Ulaya.

Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa washirika muhimu wa kibiashara na Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu ambapo inakadiriwa biashara ya mafuta ya zaidi ya dola 65 za marekani ilifanyika mwaka 2015. Kwa mwaka huo huo Nchi za Falme za Kiarabu ilikuwa miongoni mwa nchi kubwa ikishika nafasi ya nane  inayofanya biashara na Ulaya huku Umoja wa Ulaya ikiwa ya 13 kwa kufanya biashara kimataifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad