728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, November 15, 2016

  ETIHAD YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA DARAJA LA KWANZA NA WASAFIRASHAJI BORA WA MIZIGO KWA AFRIKA YA KATI NA AFRIKA KWA UJUMLA.

  Shirika la Ndege la Etihad limeshinda tuzo ya ubora ya usafirishaji kwa daraja la kwanza na wasafirishaji bora wa mizigo kwa ndege katika Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika kwa ujumla kupitia tuzo za ubora za  AirlineRatings.com 2017. Shirika hilo lenye makao makuu yake makuu Abudhabi, pia limetajwa kuwapo kwenye kumi bora duniani kutokana na ubora wa hali ya juu wa huduma zake.

  Mhariri Mtendaji wa AirlineRatings.com, Geoffrey Thomas alisema,” Shirika la Ndege la Etihad limeibuka mshindi wa tuzo hizo na kuwa mshindi wa kwanza kwa utoaji huduma daraja la kwanza na usafirishaji wa mizigo Mashariki ya kati na Afrika kwa ujumla pamoja na kuingia kwenye kumi bora za AirlineRatings.com ulimwenguni kote, kutokana  na ubora wa huduma zake.”

  Alisema, “Hili ni jambo la kujivunia kwa kushinda tuzo ya Airlineratings.com na Shirika la ndege la Etihad ndilo limeingia kwenye kumbukumbu ya kushinda maeneo matatu tofauti kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo”

  “Shirika hili la ndege limekuwa la kipekee pia kwa kufanikiwa kupata hadhi ya juu kwa bidhaa na usalama kupitia Airlineratings.com,” alisema.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “ Ushindi wa tuzo hii ya ubora kwa daraja la kwanza na wasafirishaji mahiri wa mizigo Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika kwa ujumla kwa miaka mitatu mfululizo ni jambo kubwa la heshima kuendelea kujizatiti na kuongoza kwenye ubora wa bidhaa, huduma zinazotolewa za kiwango cha juu ulimwenguni.”

   “Zawadi hii inatuhamasisha kuendelea kufanya vyema katika sekta ya anga na kuongeza ubunifu na utendaji kazi pamoja na kuimarisha usalama, jambo ambalo linatufanya kuendelea kuwa wa kwanza kwa ubora,” alisema.

  Tuzo ya The 2017 AirlineRatings.com imekuja ikiwa ni baada ya wiki chac he zilizopita baada ya kupokea nyingine kutoka kwa Skytrax Certified 5-Star Airline Rating. Tuzo hizo za Skytrax  zilizopatikana hivi karibuni zilitolewa kwa shirika hili; Shrika la ndege lenye huduma za daraja la kwanza, ubora kwenye huduma za chakula ndani ya ndege, ubora kwenye mandhari ya ndani ya ndege kwa ndege ya A380 iliyotolewa Julai 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ETIHAD YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA DARAJA LA KWANZA NA WASAFIRASHAJI BORA WA MIZIGO KWA AFRIKA YA KATI NA AFRIKA KWA UJUMLA. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top