JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ETIHAD CARGO YASAFIRISHA FARASI 72 KWENYE NDEGE MOJA

Share This
Mtaalamu wa farasi akiwa na mnyama huyo muda mfui kabla ya kumpakiza kwenye ndege 
Vyumba maalumu 24 vilivyotengenezwa kwa ajili ya kubeba farasi hao tayari kwa safari ya Kuwait

KITENGO cha Usafirishaji Mizigo cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Cargo) kimepiga hatua kubwa na muhimu katika sekta ya usafirishaji kutokana na kuanza kusafirisha  farasi zaidi ya 70 kutoka Uingereza kwenda Kuwait baada ya kumalizika msimu wa mashindano ya mbio za farasi.

Zaidi ya farasi 72 wenye thamani ya shilingi 163 sawa na Dola 36 milioni walisafirishwa kutoka Uwanja wa Ndege wa London Stansted kwenda  jijini Kuwait ambako watakuwapo huko kwa mafunzo maalumu hasa katika kipindi hiki cha baridi kali na kuzoea mbio kwenye mazingira ya joto katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Farasi hao walisafirishwa na ndege ya Boeing 777yenye hadhi ya juu ikiwa na sehemu maalumu kwa ajili ya kuwahifadhi zaidi ya farasi 75 kwa wakati mmoja.

Naibu Makamu wa Rais wa Kitengo cha Usafirishaji wa Shirika la Ndege la Etihad, David Kerr alisema, “ Usalama ni jambo la muhimu kwetu kwa wateja wetu ndio maana tunawahakikishia usalama na huduma nzuri wasafirishaji wanaotumia huduma zetu.”

Aliongeza kuwa, “Mashariki ya Kati wamekuwa na historia ya kipekee kwa miaka mingi iliyopita kwa kuwa na mizigo mingi yenye thamani kubwa tunayobeba. Kwa mwaka huu pekee kitengo chetu cha usafirishaji kimesafrisha takribani  farasi 1,200 kukiwa pia na idadi nyingine kubwa tunayotarajia kusafirisha kabla ya kuisha mwaka huu.”

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji katika Uwanja wa Ndege wa London Stansted, Conan Busby alisema, “ Tunalishukuru Shirika la Ndege la Etihad kwa kuwa shirika pekee lililojitokeza kubeba mizigo yenye thamani na inayohitaji umakini wa hali ya juu. Uwanja wa Ndege wa Stansted ndiyo wa kwanza kwa kufanya shughuli za usafirishaji wanyama hawa kwa kila mwaka. Farasi wengi walisafirishwa mwaka huu kutokana na kwenda kushiriki mashindano ya olympi na sherehe za maadhimisho ya miaka 90 ya Malkia wa Uingereza Queen Elizabeth.

Timu ya wataalamu sita walitembelea kitengo cha usafirishaji uwanjani hapo ili kuhakikisha farasi hao wanasafirishwa katika hali ya usalama wawapo kwenye ndege mpaka wanapowasili Kuwait

Farasi hao walipowasili kwenye uwanja wandege wa Stansted waliingizwa kwenye vyumba maalumu ndani ya ndege vilivyoandaliwa maalumu vyenye kuchukua farasi watatu. Mamlaka ya Usafirishaji nchini humo iliidhinisha usalama wa kusafirisha farasi hao baada ya kuridhishwa na kiwango cha joto kwa wanayama hao wawapo ndani ya ndege kwa safari inayotumia masaa takriban sita.

Kitengo cha Usafirishaji cha Shirika la Ndege la Etihad kina jumla ya ndege tisa ambazo tano ni boing 777Fs na nne kati ya hizo ni Airbus A330Fs ambazo zinauwezo wa kubeba farasi kati ya 75 na 30 kwa kila moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad