728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 23, 2016

  TANZIA: MZEE HAMADI KILUVIA AFARIKI DUNIA

  Familia ya Kiluvia ina masikitiko makubwa kutangaza kifo cha baba yao mpenzi Mzee Hamadi Kiluvia (pichani) kilichotokea alfajiri ya leo jijini Dar es salaam. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Migombani Regent Estate nyumba namba 7 ambapo ndipo ulipo msiba.

   Msibani hapo ni hatua chache kutoka kituo cha mafuta cha Oil Com Victoria house ambapo unafuata barabara ya Mikocheni kwa Kairuki hadi njia panda ambapo unakata kulia na mbele tena unakata kulia utakuwa umefika.

  Marehemu Mzee kiluvia atakumbukwa kama mmoja wa viongozi wa zamani serikalini na michezoni, ambapo katika uhai wake aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya, mmoja wa viongozi wa chama cha mpira wa miguu cha FAt enzi hizo pamoja na kuwa kiongozi aliyeheshimika sana katika klabu ya Yanga.

  Inna lillahi wa ina ilaihi rajiun
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANZIA: MZEE HAMADI KILUVIA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top