728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, September 6, 2016

  WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI.

  Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat
  Mfumukeko.

  Na Woinde shizza,Arusha.
  Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
  wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo
  kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

  Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya
  ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

  Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama
  wanadai Juni 17, Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya
  ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya
  Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza
  wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za
  wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

  Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye
  notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa
  saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina
  fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka
  Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top