KATIKA kusherekea siku ya mtoto wa Africa, Benki ya CRDB Tawi la Mlimani City limetoa zawadi mbalimbali kwa watoto na kimama waliojifungua siku ya leo.
Zawadi hizo zilizolenga kutambua mchango wa watoto wa kiafrica ambao ndio wajenzi wa taifa pamoja na wateja wa baadae wa taasisi za kibenki.
“Katika kusherekea siku hii adhimu na muhimu, Benki ya CRDB kupitia tawi lake la Mlimani City tumekuja kutoa zawadi kwa mama zetu hawa maana huwezi kusherekea siku ya mtoto bila kumpongeza na mama pia pamoja na kuwatakia kila la kheri wale ambao wanatarajia kujifungua,” alisema Mkurugenzi wa tawi hilo, Allen Kilango.
Zawadi hizo zenye thamani ya shillingi million 3.2 zilitolewa katika hospitali ya Sinza Palestina. Tawi hilo lilitoa sukari, maji, sabuni za kufulia, majani ya chai, Pampas pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya kuwatunza watoto wachanga.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine waliopo wodini, Tunu Tebesi amesema wanashkuru sana kwa msaada huo na umewapa moyo sana kama wamama na pia kuwasaidia watoto wao maana wengine walikuwa hawana uwezo wa kununua baadhi ya vitu walivyopewa.
Katika siku hiyo ya mtoto wa Africa leo, jumla ya watoto 45 walizaliwa katika hospitali hiyo jana, wakiume wakiwa 15 na wakike 30.
Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango akitoa msaada wa Pampers kwa mama aliyejifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Palestina jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City wakipangapanga vitu vya msaada wakati walipotembelea katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa tawi hilo, Bw Allen Kilango watatu kutoka kushoto akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam leo katika hospitali ya Palestina-Sinza.
Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango akitoa msaada wa Pampers kwa mama aliyejifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam leo.
Meneja uhusiano wa wateja wajasiriamali wa Benki ya CRDB Tawi la Mliamani City, Martha Ngowi akitoa msaada kwa kinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam.
Afisa wa benki ya CRDB Tawi la Mlimani City, Fatma Tinna akitoa msaada kwa mama aliyejifungua leo katika hospital ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
Meneja uhisiano wa wateja binafsi Stephen Makundikushoto msaada kwa mama aliyejifungua leo katika hospital ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila Juni 16 kila mwaka.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Palestina-Sinza jijijini Dar es Salaam leo walipo tembelewa na wafanyakazi wa benki hiyo.
No comments:
Post a Comment