Sehemu ya wadau wa mawasiliano wakimsikiliza mkuu wa mkoa hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa wadau mawasiliano juu uzimwaji wa simu feki leo katika ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Watanzania wametakiwa kutumia simu zenye viwango na kuachana simu bandia ambazo hata kiafya si salama kwa matumizi ya binadamu.
Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati mkutano wa wadau wa mawasiliano kuelekea uzimaji wa simu leo usiku wa kuamkia kesho, Makonda amesema TCRA imethubu kutoa huduma bora kwa wananchi katika mawasiliano.
Amesema TCRA imeweza kupambana tangu uzimaji wa analojia kuingia digitali ambapo Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa vitendo katika masuala mawasiliano.
Makonda amesema hata katika sheria ya mtandao baadhi ya watu walikuwa wanapinga ili kuweza kuendelea kutukana katika mitandao ambapo TCRA imeweza kufanikiwa kufanya hivyo.
Makonda amewataka wadau kuja na mawazo ya kuboresha huduma ya mawasiliano nchini katika ulinzi wa taifa.
No comments:
Post a Comment