JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WASANII 74 WAOMBA KUSHIRIKI TAMASHA LA AMANI

Share This
Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Amani, Alex Msama.

Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Amani, imesema inapata wakati mgumu kuhusiana na idadi ya waimbaji ambao wanaomba kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4, mwaka huu.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama amesema wiki hii kuwa idadi ya wanaoomba washiriki tamasha hilo imekuwa kubwa kuliko kawaida, ambapo hadi juzi walikuwa waombaji wamefikia 74.
 
“Tunapata maombi mengi, tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kujipanga ili kuweza kila mmoja ashiriki, lakini tuna vigezo ambavyo tunaviangalia kwanza,” alisema.
 
Msama amesema tamasha hilo pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afrika Kusini na Zambia.


"Waimbaji wengi maarufu wa muziki wa injili watakuwepo, tumejipanga vizuri kuhakiksha tamasha hili linakuwa gumzo kila mahali.

"Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kwa vile kutakuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho," alisema Msama.

Msama amesema lengo la kuwajumuisha wasanii hao ni kutaka kulifanya tamasha hilo lenye lengo la kuombea amani liwe bora na lenye tija kwa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad