JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TAMASHA LA MUZIKI MNENE BAR KWA BAR KUFANYIKA JUMAMOSI MKURANGA MKOANI PWANI

Share This
 Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Sadiq (kushoto), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kabla ya kumkaribisha Meneja wa Mawasiliano wa redio hiyo kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la muziki mnene bar kwa bar litakaloanza kesho kutwa Jumamosi, Agosti 5, 2015 Mkuranga mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama na katikati ni Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo. Kampuni ya simu ya Smart wamedhamini tamasha hilo.
 Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama.
 Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.


 Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), na Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama, wakiwaonesha moja ya jezi zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya tamasha hilo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.


 Dotto Mwaibale

TAMASHA la Muziki Mnene Baa kwa Baa linatarajia kuanza kufanyika jumamosi ya Septemba 5, mwaka huu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo alisema kuanza kwa tamasha hilo kesho ni baada ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Mtaa kwa Mtaa awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji wengi wa EFM wameweza kujishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya wapenzi wa burudani na mambo ya party.


Ssebo amesema Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na sasa wameamua kuupekea katika mkoa wa Pwani.

Ametaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Rdjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  

Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.

Ameongeza kuwa Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu utaanza rasmi kesho jumamosi Mkuranga ambako mbali na kutoa Burudani, wataanza na mchezo wa mpira ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kujumuika nasi tuonane nao mchana. 


Ssebo amesema  mwishoni watafanya Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.


“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana 

tutawafikia na kuwamiminia burudani ambayo pia itarushwa live 
kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo 
tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu 
Muziki unaongea”. 

Muziki mnene awamu hii  umedhaminiwa na kampuni ya simu mpya kabisa hapa Tanzania ya Smart, kampuni ambayo  huduma zake ni za gharama ndogo zaidi, kwa hiyo mwaka huu Smart watakuwa na sisi katika kuupeleka  Muziki Mnene bar kwa bar kwa mashabiki wa EFM. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad