JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA INAYOENDESHWA NA UTT AMIS YAPATA FAIDA KUBWA

Share This
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa UTT AMIS Bw.Simon Migangala akiongea na waandishi wa habari jana Dar es salaam kuhusiana na ufanisi wa mifuko kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

UTT AMIS ndiyo waendeshaji na waanzilishi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini.Mpaka sasa wanaendesha mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya shilingi bilioni 227.

Bwana Migangala aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa ujumla ukuaji wa mifuko umekua mzuri na umewezasha kutoa faida nzuri kwa wawekezaji wake zaidi ya 100,000 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mfuko uliotoa faida nzuri zaidi ni Mfuko wa Watoto ambao ulitoa asilimia 51.19 ukifuatiwa na Wekeza Maisha uliotoa asilimia 45.23

Mfuko wa tatu ni Umoja ambao ulikua kwa asilimia 38.46, wanne Kujikimu alikua kwa asilimia 36.77 na Ukwasi kwa asilimia 11.46

Alisema kimsingi wanafurahia na wanajivunia faida hiyo waliyopata wawekezaji wao.Ukuaji huu umechangiwa na ufanisi mzuri wa soko la Hisa la Dar es salaam , masoko ya fedha ambako mifuko pia huwekeza na weledi wa meneja wa Mifuko (UTT AMIS) katika kuwekeza na kusimamia mifuko.

Katika kipindi hicho cha miezi sita thamani halisi za vipande vya mifuko viliongezeka kama ifuatavyo;

Kipande cha Mfuko wa Umoja kiliongezeka kutoka shilingi 365.6892 hadi shilingi 435.9008,Wekeza Maisha kilitoka shilingi 237.5386 hadi 291.1558 kwa Mfuko wa Watoto kiliongezeka kutoka shilingi 213.72 hadi shilingi 268.3172

Mfuko wa Kujikimu kutoka shilingi 118.1779 hadi shilingi 131.1440(ukijumuisha na gawio la shilingi 4 kila baada ya miezi mitatu) na mwisho Mfuko wa Ukwasi toka shilingi 114.3608 hadi shilingi 120.9362.

Ongezeko hilo linathibitisha ukuaji wa mifuko yetu na tunawahamasisha watanzania wajiunge katika mifuko hii waweze kuwekeza fedha zao na kupata faida maridhawa.Tunaendelea kuwaambia kuwa ni fedha zako,ni akiba yako,ni uwekezaji wako, faida ni yako! UTT AMIS tunawezesha! Hakika tutaendelea kuwa ‘Mshirika hakika katika uwekezaji’

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad