JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAKALA YA SHERIA: JE INARUHUSIWA KUINGIZA MALI YA WANANDOA KATIKA MALI ZA MIRATHI ILI NDUGU WAZIGAWANE IWAPO MKE/MME AMEFARIKI

Share This

Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi kila inapotoka makala. Nami nimeweka ahadi ya kukusanya maswali hayo na kuyajibu na si kuyajibu kwa kumjibu mtu aliyeuliza peke yake , hapana isipokuwa kwa kuyaweka katika makala ili umma wote ufaidike. Haya ni baadhi ya maswali ambayo nimeulizwa na haya ndiyo majibu yake.

1.JE MALI ALIYOPEWA MTU KABLA YA KIFO CHA MAREHEMU NAYO HUHESABIWA KATIKA KUGAWANA MIRATHI.

Yapo mazingira ambapo marehemu huwa amempa mtu/mrithi mali kabla ya kifo. Mara nyingi hii hujitokeza kwa baba au mama na mtoto ambapo baba/mama humpa mali mwanae hata kabla ya kifo. Hampi ile mali kama amemrithisha hapana isipokuwa anaweza kumpa sehemu ya mali pengine ili ajenge au sehemu ya shamba ili alime na wengine huwa wametoa vitu kama magari au hata nyumba. Swali ni je iwapo mtu amepewa vitu kama hivi au amepewa kimojawapo kati ya hivi ni sawa vitu hivi alivyopewa kuhesabiwa wakati wa kugawana mali za marehemu aliyempa mali hizo. Jibu ni ndiyo, sheria inasema iwapo marehemu hakuacha wosia basi wakati wa kugawana mali zake vile vitu ambavyo alivitoa kwa baadhi ya watu/ warithi yafaa vihesabiwa wakati wa mgawanyo wa mali.

Sio kwamba mtu atanyanganywa mali hizo hapana isipokuwa aliyekwishapewa hawezi kupata mgao sawa na yule ambaye hakuwahi kupewa chochote na marehemu wakati wa uhai. Ambaye hakuwahi kupewa chochote yafaa apate mgao zaidi kuliko yule aliyekuwa amepewa na marehermu kabla ya kifo. Isipokuwa hali itakuwa tofauti iwapo marehermu ameacha wosia. Ikiwa marehemu ameacha wosia basi kila mtu atapata kutokana na wosia unavyosema bila kujali nani alikuwa amepewa kabla na nani hakupewa kabla. Wosia utafuatwa hivyohivyo ulivyo.

2. JE INARUHUSIWA KUINGIZA MALI YA WANANDOA KATIKA MALI ZA MIRATHI ILI NDUGU WAZIGAWANE IWAPO MKE/MME NDIYE AMEFARIKI.

Yapo mazingira ambapo mke anaweza kumtangulia mume katika mauti au mme anaweza kumtangulia mke . Lakini mpaka kifo kinamkuta mmoja unakuta tayari kuna mali ambazo zilikuwa zimechumwa na wanandoa kwa pamoja na hivyo kuwa mali za familia. Hapo hapo unakuta kuna warithi kama watoto au ndugu wengine na wanataka mali zote ziingizwe katika orodha ya mirathi na zigawanywe. Swali ni je sheria inasemaje kuhusu jambo hilo. Sheria iko wazi kuwa katika mazingira kama hayo huwezi kuingiza mali zote kwenye mali za mirathi. Kinachotakiwa kufanyika ni kutoa kiwango cha mgao wa mali ambao alikuwa anastahili marehemu kama mgao wake katika mali kama mwanandoa .

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad