JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WADAU TAREA WAOMBA MASHAURIANO TRA, TBS NA WIZARA

Share This
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) jijini Dar es Salaam pamoja na Wageni waalikwa meza kuu kwenye uzinduzi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio akizungumza na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) alipokuwa akifungua rasmi Madhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), Dk. Prosper Magali akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) uliofanyika jijini Dar es Salaam sambamba na Maadhimisho ya Miaka 25 ya TAREA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio (kushoto) akiwa kwenye Banda la Kampuni ya Rex Energy kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Operesheni Meneja wa REX ENERGY, Bi. AGNES KIBHISA akishuhudia.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipotembelea Banda la Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) uliofanyika Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa TAREA, MHANDISI DK. MATHEW MATIMBWI akishuhudia.

Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya ENSOL TANZANIA LIMITED, Bi. Zahra Lupatu akitoa maelezo Kwa Katibu MKUU wa WIZARA ya Nishati, Dk. James MATARAGIO katika Maonesho ya WIKI YA NISHATI JADIDIFU 2026, Jijini DAR ES SALAAM.


Na Mwandishi Wetu, Dar

WADAU wa Jumuiya ya Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) wameshauri uwepo wa mashauriano endelevu baina yao na Serikali  kupitia, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuchochea mabadiliko.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TAREA, Dk. Prosper Magali mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio kwenye hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania kwa Mwaka 2026 (REW 2026) uliofanyika jijini Dar es Salaam sambamba na Maadhimisho ya Miaka 25 ya TAREA.

Alisema mashauriano hayo na taasisi hizo yatachochea Watanzania kufikia lengo la Serikali katika Mkakati wake wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia inafikia asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034.

“Tunaomba mashauriano endelevu kati ya Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ofisi ya Viwango ya Tanzania na sekta binafsi kabla ya hatua za kifedha zinazoathiri teknolojia za nishati mbadala na ufanisi wa nishati kuletwa au kubadilishwa,” alisema.

Aidha aliongeza kuwa Sera na udhibiti wa kodi; kuimarisha ushiriki wa kampuni ya Tanzania katika programu kuu za nishati na umuhimu wa mbinu makini ya ruzuku, hasa katika matumizi ya nishati safi na endelevu pia kutachochea malengohayo.

Dk Magali, alibainisha kuwa uwekezaji wa nishati jadidifu na ufanisi wa nishati ni wa muda mrefu, hivyo kampuni huagiza vifaa, huanzisha mitandao ya usambazaji, huajiri mafundi, huwekeza katika vifaa na huingia katika mipango ya ufadhili kulingana na hali inayotarajiwa ya soko.

“Hivyo, mabadiliko ya mara kwa mara au yasiyotabirika katika kodi, ushuru, uainishaji na taratibu za utekelezaji huongeza hatari ya uwekezaji na hatimaye huongeza gharama kwa watumiaji,” alisema na kuongeza kuwa, utekelezaji wa misamaha ya kodi inayoidhinishwa unaweza kuongeza chachu ya mafanikio.

“Serikali imnapoidhinisha misamaha ya kodi kwa vifaa vya nishati jadidifu, nishati safi ya kupikia au vitu vinavyotumia nishati kwa ufanisi, misamaha hiyo inapaswa kutumika waziwazi na kwa uthabiti katika mchakato mzima wa uingizaji na utekelezaji, Msamaha uliopo katika sera, lakini ni mgumu kupatikana kivitendo haufikii lengo lililokusudiwa.”

Magali alisema suala la mitaji pia ni changamoto nyingine kwani taasisi nyingi za fedha ziokiwamo benki zinmenga fedha, lakini masharti ya kuzifikia ni magumu na yanawashinda wadau wengi wa nishati jadidifu.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo, Dk Mataragio aliyekuwa mgeni rasmi alisema suala la kuongeza ufanisi katika mifumo ya usambazaji na kupunguza upotevu wa umeme bado ni kipaumbele.

“Natoa wito kwa viwanda, biashara, taasisi za umma, kaya, wasimamizi, wazalishaji na watoa huduma za teknolojia kufanya suala la ufanisi wa nishati kuwa sehemu muhimu ya shughuli zao. Ufanisi wa nishati si tu kuhusu kuokoa umeme, bali pia kuboresha uzalishaji, kupunguza gharama za uendeshaji na kuimarisha usalama wa nishati ya taifa.”

Dk. Mataragio ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, alisema Serikali inalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini kufikia Megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030.

Alisema megawati 1,892 zinatarajiwa kuzalishwa kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati jadidifu kama vile jua, biomasi na upepo.

Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu: 'Kutoka Dira Hadi Matokeo: Ubunifu, Ushirikiano na Kasi kuelekea Tanzania ya Kijani,” Kamishina Msaidizi wa Nishati Jadidifu Wizara ya Nishati, Imani Mruma alisema inaakisi mwelekeo wa Tanzania kubadilisha sekta yake ya nishati.

“Kama nchi, tumeweka malengo makubwa ya maendeleo chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwemo kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme kufikia angalau megawati 8,000 (MW) ifikapo mwaka 2030 na kulenga kufikia takriban megawati 70,000 (MW) ifikapo mwaka 2050.”

Alisisitiza kuwa kufikia malengo hayo kunahitaji mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya nishati, uwekezaji zaidi katika nishati mbadala, miundombinu imara ya umeme, ubunifu wa kiteknolojia, pamoja na ushirikiano madhubuti kati ya serikali na sekta binafsi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad