JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


URASIMISHAJI VWA MATUMIZI YA MBEGU ZA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA (TARI)

Share This

 


Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inapenda kuwataarifu wadau wote
wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mbegu zinazomilikiwa na
Taasisi kuwa ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia taratibu za haki miliki, ikiwemo

kusaini mikataba rasmi ya matumizi (Licensing Agreements) na kulipa mirabaha stahiki kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 30 vikisomwa pamoja na Kifungu cha 40 cha Sheria ya Haki Miliki za Ugunduzi wa Mbegu za Mimea (Plant Breeders' RightsAct), pamoja na Kanuni ya 33(b) ya Kanuni za Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania, 2023, TSN. 448 la tarehe 30 Juni 2023.

Kwa mantiki hiyo, TARI inatoa wito kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji, kampuni, taasisi na mtu yeyote anayejihusisha au anayetarajia kuanza kuzalisha, kusambaza au kuuza mbegu au teknolojia nyingine yoyote inayomilikiwa na TARI, kuwasiliana na

Taasisi ndani ya kipindi cha siku thelathini (30) na kipindi hicho cha siku 30 kikiisha, TARI itachukua hatua za kisheria dhidi ya wadau wote watakaoshindwa kutekeleza wito huu. Lengo la tangazo hili ni kuwataka wadau:

. Kujisajili

i. Kuhakiki na kuhuisha taarifa zao
i. Kusaini mikataba rasmi ya matumizi ya teknolojia na mbegu za TARI; na
İv. Kuweka utaratibu sahihi wa ulipaji wa mirabaha kwa mujibu wa Sheria na Kanuni.
Taarifa hili imetangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Namba.18012 la tarehe 9

Oktoba, 2026.
Taarifa ziwasilishwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi Mkuu,

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI),

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad