JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO III KUINUA UZALISHAJI WA KILIMO

Share This

 


ONGEZEKO la mradi wa umwagiliaji Idudumo III  uliopo Nzega, mkoani Tabora kutoka hekta 173 hadi kufikia hekta 1,500 umepongezwa kwa kulenga kuchochea kasi ya uzalishaji wa mazao na kuleta tija ya kiuchumi kwa wakulima. 

Hayo yamesemwa tarehe 2 Oktoba 3026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Philip Mwanyika (Mb) wakati wa ziara ya kikazi mkoani humo.  Ameipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NiRC) chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Raymond Mndolwa kwa kuhakikisha mradi huo unasimamiwa kwa  thamani halisi ya fedha  ambapo wanufaika ni wananchi wa Nzega, mkoani Tabora.

“Miradi hii inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi na kutoa fursa kubwa za kiuchumi. Ni muhimu wananchi watambue kuwa miundombinu hii ni ya kwao na wanapaswa kushiriki kikamilifu katika kuitunza na kuchangia huduma kwa mujibu wa sheria ili iweze kudumu na kuleta tija iliyokusudiwa,” amesema Mhe. Mwanyika.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni azma ya Serikali ya kuimarisha usalama wa chakula kwa kuleta mapinduzi katika Sekta ya Kilimo kupitia umwagiliaji, akibainisha kuwa uwekezaji huo unalenga kumkomboa mkulima mdogo na kukuza uzalishaji wenye tija.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad