JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MKUYU AFRICA YAPELEKA KARIAKOO NA MASAKI DUBAI

Share This

Kampuni ya Mkuyu Africa imewaleta karibu Watanzania wanaofanya shughuli mbalimbali nchini Dubai kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania, hususan katika sekta ya ardhi na majengo.

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo biashara na mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Dubai yakiendelea kukua, huku wafanyabiashara wengi kutoka Tanzania wakifika katika nchi za Falme za Kiarabu, hasa Dubai, kutafuta bidhaa na fursa za biashara, ikiwamo nguo, bidhaa za thamani na mapambo ya ndani pamoja na kazi za viwandani.

Katika kuunga mkono jitihada hizo, MKUYU AFRCA  iliandaa kongamano lililowakutanisha wafanyabiashara wadogo wenye asili ya Tanzania wanaoishi Dubai, ambapo walijadili namna wanavyoweza kutumia fursa wanazozipata ughaibuni kuwekeza nyumbani.

Lengo lingine la kongamano hilo lilikuwa kuwapa washiriki uelewa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya ujenzi na mali isiyohamishika, pamoja na namna Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanavyoweza kumiliki mali nchini kupitia mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi wa Mkuyu Africa, Juneid Othman, alisema Watanzania waliotoka nchini miaka 10 iliyopita wanaweza kushangazwa na kasi ya maendeleo katika sekta ya ujenzi nchini.

Alisema sekta hiyo imekua kwa kiasi kikubwa, ikiwamo ujenzi wa majengo marefu, nyumba za makazi na miradi ya nyumba za kupangisha, hasa katika maeneo ya kibiashara kama Kariakoo chini ya mradi wa Nkurumah  na maeneo ya kifahari kama Masaki.

“Ukitoka Tanzania miaka 10 iliyopita na ukarudi leo, unaweza kushangazwa na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika sekta ya ujenzi. Kuna maendeleo makubwa katika ujenzi wa majengo ya biashara, makazi na nyumba za kupangisha,” alisema.

Juneid alisema pia mazingira ya uwekezaji yameendelea kutoa fursa kwa Watanzania kumiliki mali kupitia benki na taasisi mbalimbali za kifedha.

Alitoa mfano wa miradi ya Mkuyu Africa katika maeneo ya Kariakoo na Masaki, akisema kampuni hiyo inaendelea kushiriki katika ujenzi na uendelezaji wa majengo ya makazi na biashara.

Alisema fursa hizo zinapaswa kutumiwa na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, akisisitiza kuwa uwekezaji katika mali nchini unaweza kuwa sehemu ya maandalizi ya maisha yao ya baadaye pamoja na kujenga urithi kwa vizazi vijavyo.

Wafanyabiashara Dubai wataka kuwekeza nyumbani

Mfanyabiashara wa bidhaa za thamani na mapambo ya ndani nchini Dubai, Ashraf Mohamud, alisema Watanzania wengi wanaoishi Dubai wanaendelea kufanya biashara na kutafuta mitaji kwa lengo la baadaye kuwekeza nchini.

Alisema ujio wa Mkuyu Africa nchini Dubai umewapa motisha na taarifa zaidi kuhusu fursa zilizopo nchini, jambo ambalo, kwa mujibu wake, linawasaidia kupanga namna ya kuanza kuwekeza nyumbani.

“Tumekuja Dubai kutafuta maisha na kufanya biashara, lakini moja ya malengo yetu ni kupata mtaji na kuja kuwekeza nyumbani. Ujio wa Mkuyu Africa umetupa hamasa na kutufanya tuanze kufikiria kwa umakini zaidi kuhusu uwekezaji nchini,” alisema.

Malipo kwa awamu

Ashraf alisema Watanzania wengi wanaoishi Dubai wana hamu ya kuwekeza Tanzania, lakini baadhi yao wamekuwa wakikumbana na changamoto pale wanapowatumia ndugu fedha kwa ajili ya kununua ardhi au kujenga nyumba.

Alisema hali hiyo imewafanya baadhi yao kutafuta njia mbadala zitakazowawezesha kufanya uwekezaji moja kwa moja na kwa utaratibu unaoeleweka.

“Watanzania wengi wanaoishi huku wanatamani kuja kuwekeza nchini, lakini hapo awali kumekuwa na changamoto na wakati mwingine urasimu, hasa pale tunapowatuma ndugu zetu fedha kwa ajili ya uwekezaji,” alisema.

Aliongeza kuwa fursa zinazotolewa na kampuni kama Mkuyu Africa, ikiwamo uwezekano wa kumiliki mali kupitia taasisi za kifedha na kulipa kwa awamu kulingana na masharti yaliyowekwa, zinaweza kuwasaidia Watanzania waishio nje ya nchi kuwekeza kwa utaratibu rasmi.

Kwa mujibu wa washiriki wa kongamano hilo, uwekezaji nchini Tanzania unapaswa kuonekana kama sehemu ya kujenga maisha ya baadaye, kuongeza thamani ya mitaji na kuweka msingi wa mali kwa ajili ya familia na vizazi vijavyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya MKUYU AFRICA ,Juneid Othmani akizungumza wakati wa kongamano la wafanyabiashara wenye asili ya Tanzania  waishio Duba


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad