
MACHO ya mashabiki wa soka nchini Hispania yataelekezwa katika dimba la Sevilla, ambapo Sevilla FC itakuwa mwenyeji wa CA Osasuna katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga), unaotarajiwa kuanza saa 17:00 Jioni. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikihitaji matokeo mazuri ili kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa ligi.
Sevilla wataingia katika mchezo huo wakitafuta kutumia faida ya kucheza nyumbani, ambako watahitaji kuungwa mkono na mashabiki wao ili kupata matokeo chanya. Timu hiyo inahitaji kuwa makini katika kutumia nafasi za kufunga na kuepuka makosa ya kujilinda ambayo yanaweza kuwapa wapinzani nafasi ya kupata mabao.
Kwa upande wa Osasuna, timu hii unaingia kwenye mchezo huu huku ikiwa na matumaini ya kuendeleza matokeo mazuri baada ya kuifunga Racing Santander mabao 2-0 katika mchezo wake uliopita.
Ushindi huo unaweza kuwapa wachezaji morali ya kupambana dhidi ya Sevilla, huku mshambuliaji Ante Budimir akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuwa tishio kwa safu ya ulinzi ya wenyeji kutokana na uwezo wake wa kutumia nafasi za kufunga.
Takwimu za msimu zinaonyesha Sevilla ikiwa na pointi 14 baada ya michezo tisa, huku Osasuna ikiwa na pointi 11 katika idadi hiyo hiyo ya michezo. Hata hivyo, Sevilla inahitaji kuboresha safu yake ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao mengi katika baadhi ya michezo ya hivi karibuni, wakati Osasuna nayo italazimika kuwa imara ili kuzuia mashambulizi ya wenyeji.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.


No comments:
Post a Comment