JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TRAMEPRO Yatoa Salamu za Rambirambi kwa Mh. Rais Samia

Share This

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM: Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO), Boniventura F. Mwalongo, ametoa salamu za pole na rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Hafidh Ameir.

Katika salamu zake, Mwalongo ameeleza masikitiko na huzuni kubwa kufuatia msiba huo, huku akimtakia Rais Samia, watoto, familia, ndugu, jamaa pamoja na wote walioguswa na msiba huo kupata faraja, nguvu, subira na moyo wa uvumilivu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Amesema katika kipindi hicho kigumu cha majonzi, familia inahitaji nguvu na faraja ili kukabiliana na wakati huo wa huzuni.

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu, kwa rehema na upendo wake, ailaze roho ya Marehemu mahali pema na amsamehe makosa yake yote. Amina,” amesema Mwalongo.

Ameongeza ujumbe wa pole kwa Rais Samia, familia pamoja na Taifa kwa ujumla, akiwataka kuwa na moyo wa subira katika kipindi hicho cha majonzi.

“Pole sana Mheshimiwa Rais. Pole kwa Familia. Pole kwa Taifa. Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki cha majonzi,” amesema.

Boniventura F. Mwalongo Katibu Mkuu – TRAMEPRO

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad