JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


PROF. NOMBO ATEMBELEA BANDA LA TUME YA TAIFA YA UNESCO MAONESHO YA WIKI YA ELIMU,TANGA

Share This

 

Na Julitha Mlay ,NATCOM
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa yanayoendelea jijini Tanga.

Katika ziara hiyo, Prof. Nombo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo, pamoja na maudhui yanayotolewa kwa umma kuhusu UNESCO, majukumu ya Tume na programu zake katika maeneo ya elimu, sayansi, utamaduni, mawasiliano na taarifa.

Prof. Nombo aliambatana na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi, Dkt. Fredrick Salukele, ambapo walipata maelezo kuhusu namna Tume inavyotumia majukwaa ya kitaifa kuwafikia wananchi, wanafunzi, walimu, vijana na wadau mbalimbali kwa kuwapatia taarifa kuhusu UNESCO na fursa zinazopatikana kupitia programu zake.

Ushiriki wa Tume ya Taifa ya UNESCO katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa wa umma kuhusu UNESCO, pamoja na kuonesha mchango wa elimu, sayansi, utamaduni, mawasiliano na taarifa katika kukuza maarifa, ubunifu na maendeleo endelevu nchini.

Kupitia maonesho hayo, Tume inaendelea kuwafikishia wananchi taarifa kuhusu kazi za UNESCO na maeneo mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa programu zake nchini Tanzania, huku ikihamasisha jamii kutumia maarifa na fursa zilizopo kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa yanaendelea jijini Tanga yakishirikisha taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, ujuzi na ubunifu, kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu fursa, huduma na jitihada zinazochangia maendeleo ya rasilimali watu nchini



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad