Na Mwandishi Wetu
NIC Insurance imewahimiza wananchi kutumia fursa ya Bima ya Maisha ya Majaliwa katika kujiwekea malengo ya kifedha yatakayowasaidia baada ya kufikia muda walioujiwekea.
Hayo yamesemwa na Afisa Bima wa NIC Insurance, Thecla Mtege, wakati akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la NIC Insurance katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.
Thecla amesema kupitia Bima hiyo, mwananchi anaweza kujiwekea malengo ya kifedha kwa muda anaouona unafaa, ikiwamo miaka mitano, 10 au zaidi, huku akichangia kiasi cha fedha anachokimudu kila mwezi.
Amesema utaratibu huo unamwezesha mwananchi kuweka akiba kwa ajili ya kutimiza malengo yake ya baadaye, kulingana na kiwango na muda alioujiwekea.
“Bima ya Maisha ya Majaliwa inamwezesha mwananchi kuchangia kiasi kidogo cha fedha kila mwezi kulingana na uwezo wake na malengo aliyojiwekea,” amesema Thecla.
Aidha, amesema iwapo mwananchi aliyekata Bima hiyo atafariki kabla ya kukamilisha muda wa Bima, NIC Insurance italipa kiasi cha Bima kwa wategemezi waliotajwa kwenye taarifa za Bima kwa kiwango kilekile kilichoainishwa.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha familia ya mwananchi aliyejiwekea mpango huo inaendelea kupata ulinzi wa kifedha hata endapo atafariki kabla ya kufikia muda wa kukamilisha malengo yake.




No comments:
Post a Comment