JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MANYARA KUWAFIKIA WATOTO 670,000 KATIKA KAMPENI YA CHANJO YA POLIO

Share This





Na Mwandishi wetu, Babati

Mkoa wa Manyara umeweka mkakati wa kuhakikisha watoto 670,000 wenye umri chini ya miaka 10 wanafikiwa na kupata chanjo katika Kampeni ya Chanjo ya Polio ya Matone, huku maandalizi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Kampeni hiyoyakiendelea kufanyika mkoani humo.

Akizungumza baada ya kupata nafasi ya kuonana na Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt Georgina Joachim kutoka Wizara ya Afya pamoja na Dkt Floriani Tinuga kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, amesema mkoa uko tayari kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi.

Mhe. Sendiga amesisitiza kuwa Serikali ya Mkoa imejipanga kuhakikisha hakuna mtoto atakayeachwa nyuma, na kwamba juhudi zote zitaelekezwa katika kuwafikia watoto wote 670,000 wanaolengwa kupata chanjo kuanzia tarehe 27 hadi 30 Agosti 2026.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali, wataalamu wa afya, viongozi wa maeneo, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ni muhimu katika kuhakikisha kampeni hiyo inafikia malengo yaliyowekwa.

Kampeni hiyo inalenga kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa wa Polio kwa watoto na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto kupata chanjo kwa wakati.

Katika utekelezaji wa kampeni, timu za wataalamu wa afya zinatarajiwa kushirikiana na viongozi na jamii watapita nyumba kwa nyumba, mashuleni, kwenye minada, masoko, nyumba za Ibada na maendeo yenye mikusanyiko kuwatafuta na kuwapatia chajo walengwa wote wa zoezi hili.

Mkoa wa Manyara pia unaendelea na maandalizi kuelekea uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Polio ya Matone Kitaifa tarehe 27 Agosti 2026, huku uongozi wa Mkoa ukisisitiza utayari wake wa kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad