
NAIBU Katibu Mtendaji Tume ya Taifa ya Mipango - Biashara na Ubunifu, Dkt. Blandina Kilama amesema anaitegemea Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya maendeleo 2050 iliyoanza Julai Mosi mwaka huu.
Akizungumza katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa - Sabasaba katika banda la PURA Dkt Kilama amesema ana matumaini makubwa kwamba PURA itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha utekelezaji wa DIRA 2050 unakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Bw. Ebeneza Mollel kutoka PURA amesema kufuatia utekelezaji wa DIRA 2050 tayari PURA imehuisha Mpango Mkakati wa Taasisi kwa mwaka 2026/27 - 2030/31 ili kuendana na matakwa ya DIRA 2050.
Nishati ni moja ya kichocheo katika vichocheo vitano kufanikisha malengo ya DIRA 2050, ambapo PURA inaendelea kutoa elimu kuhusu utafutaji uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini katika Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.


No comments:
Post a Comment