Na Mwandishi Wetu
AFISA Mtendaji Mkuu wa MIXX, Angelica Pesha, amesema kampuni hiyo imejipanga kikamilifu kuwahudumia wananchi wanaotembelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha na mawasiliano kwa urahisi na usalama.
Pesha alitoa kauli hiyo alipotembelea banda la MIXX katika maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema MIXX imeweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wananchi kufanya miamala mbalimbali ya kifedha bila ulazima wa kubeba fedha taslimu, hatua ambayo inalenga kuongeza usalama na urahisi wa huduma kwa watumiaji.
"Hatuna sababu ya wananchi kutembea na fedha taslimu wakati huduma zetu zinapatikana hapa bandarini. Tunawahimiza wote wanaotembelea Sabasaba kufika banda la MIXX ili wapate huduma za kifedha kwa haraka na kwa usalama," alisema Pesha.
Aliongeza kuwa, pamoja na huduma za kifedha, MIXX pia inatoa huduma mbalimbali za mawasiliano, ikiwemo ununuzi wa bando na huduma nyingine zinazowarahisishia wateja kuendelea kuwasiliana popote walipo.
Pesha aliwataka wananchi kutumia fursa ya maonesho hayo kutembelea banda la MIXX ili kujionea huduma zinazotolewa na kupata elimu kuhusu suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazorahisisha maisha ya kila siku.
Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yamewakutanisha taasisi za Serikali na sekta binafsi zikionyesha bidhaa, huduma na ubunifu mbalimbali unaochochea maendeleo ya biashara na uchumi nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MIXX Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari walivyojipanga kuhudumia wananchi maonesho ya Sabasaba



No comments:
Post a Comment