JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Busan: Afrika Yaunga Mkono Juhudi za Tanzania Kulinda Maeneo ya Urithi wa Dunia

Share This

 


Na Mwendishi Wetu,Korea
MWENYEKITI  wa Kundi la Afrika katika Kikao cha 48 cha Kamati ya Urithi wa Dunia, Balozi Pierre Faye, ameipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuandaa kikao cha pembeni kilicholenga kujadili mustakabali wa uhifadhi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine ya Urithi wa Dunia.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Julai 27, 2026, Busan, Balozi Faye alisema mkutano huo unaendana na malengo ya Mkataba wa Urithi wa Dunia unaohimiza nchi wanachama kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa maeneo ya urithi pamoja na kuendeleza juhudi za kuyahifadhi kupitia elimu na utoaji wa taarifa.

Alisema mikutano ya aina hiyo ina nafasi muhimu ya kuwakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ili kujenga ushirikiano katika kulinda maeneo ya urithi wa asili kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Balozi Faye alieleza kuwa ingawa jukumu la msingi la kuhifadhi maeneo ya Urithi wa Dunia liko mikononi mwa nchi husika, jumuiya ya kimataifa pia ina wajibu wa kushirikiana kuhakikisha maeneo hayo yanaendelea kulindwa na kuhifadhiwa.

Aliisifu Tanzania kwa kutenga takribani asilimia 38 ya eneo lake kwa shughuli za uhifadhi, hatua iliyoifanya kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani katika kulinda rasilimali za asili.

Alitaja maeneo ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kuwa miongoni mwa maeneo ya Urithi wa Dunia yanayoifanya Tanzania kutambulika kimataifa katika sekta ya uhifadhi.

Akizungumzia Ngorongoro, Balozi Faye alisema eneo hilo linakabiliwa na changamoto zinazotokana na ongezeko la idadi ya watu, haki za wafugaji na matumizi ya ardhi, hali inayoongeza ushindani wa matumizi ya malisho na vyanzo vya maji.

Alibainisha kuwa changamoto hizo zimeweka shinikizo katika mfumo wa mwaka 1959 uliolenga kuweka uwiano kati ya shughuli za ufugaji wa jamii ya Wamaasai na uhifadhi wa mazingira.

Aidha, alisema Mkataba wa Urithi wa Dunia unatambua umuhimu wa kuwepo kwa uwiano kati ya maendeleo ya binadamu na uhifadhi wa mazingira, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ndio njia bora ya kuhakikisha Ngorongoro inaendelea kuhifadhi hadhi yake ya urithi wa kipekee duniani.

Balozi Faye alihitimisha kwa kupongeza mwitikio mkubwa wa washiriki wa kikao hicho na kutoa wito kwa wadau wote kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa njia ya kujenga ili kupata suluhisho litakalowanufaisha wananchi, uhifadhi na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad