JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RAIS MSTAAFU DKT. JK AWASILI BOTSWANA KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MAZISHI YA HAYATI FESTUS MOGAE

Share This

 


GABORONE, BOTSWANA
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili nchini Botswana leo tarehe 15 Mei 2026 kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika shughuli za Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Botswana, Hayati Festus Gontebanye Mogae.

Hayati Mogae alifariki dunia tarehe 08 Mei 2026 akiwa na umri wa miaka 86. Mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika kesho, tarehe 16 Mei 2026, jijini Gaborone.

Mara baada ya kuwasili nchini humo, Mheshimiwa Dkt. Kikwete alifika katika Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Botswana ambako alisaini katika Kitabu cha Rambirambi kuenzi mchango mkubwa wa Hayati Mogae kwa taifa la Botswana na bara la Afrika kwa ujumla.

Pichani Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Kikwete anaonekana akisaini kitabu cha rambirambi huku nyuma yake akiwa amesimama Mheshimiwa James Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Botswana.

Katika picha ya pili, Mheshimiwa Dkt. Kikwete anaonekana akiwa pamoja na Mheshimiwa Dithapelo Keorapetse, Spika wa Bunge la Botswana, pamoja na Dkt. Gabriel Goitsemodimo Gosiame Malebang, Katibu wa Bunge la Botswana.

Wengine ni Mheshimiwa Balozi James Bwana pamoja na Balozi Mstaafu Dkt. Athalia Molokomme ambaye alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana wakati wa mapokezi ya Mheshimiwa Rais Mstaafu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad