Benki ya NMB imewahimiza wanawake wajasiriamali nchini kurasimisha vikundi vyao ili waweze kutambulika kisheria na kunufaika zaidi na mikopo, elimu ya fedha na huduma nyingine za kifedha zinazolenga kuinua shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza katika hafla ya Siku ya Mama iliyofanyika jijini Dodoma, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, alisema wanawake wengi wana uwezo mkubwa wa kufanya biashara na kuchangia maendeleo ya familia na taifa, lakini changamoto ya kutokuwa katika vikundi vilivyosajiliwa imekuwa ikiwanyima nafasi ya kufikiwa kirahisi na taasisi za kifedha.
Shango alisema urasimishaji wa vikundi unaongeza uaminifu, nidhamu ya kifedha na uwezo wa wanawake kupata mikopo yenye masharti nafuu, elimu ya ujasiriamali, huduma za kidijitali na ushauri wa usimamizi wa fedha. Aliwahimiza pia kutumia mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha kwa wakati ili kujenga historia nzuri ya kifedha.
Mmoja wa wajasiriamali walioshiriki hafla hiyo, Sharifa Mohamed kutoka Sabasaba, alisema mikopo kutoka NMB imemsaidia kuongeza mtaji na kupanua biashara yake hatua kwa hatua. Aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kutoa elimu na fursa kwa wanawake, akisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuwafanya wanawake wengi kujitegemea kiuchumi na kuboresha maisha ya familia zao.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)



No comments:
Post a Comment