JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WATANZANIA WANUFAIKA NA MIRADI YA KIMKAKATI NA UWEKEZAJI

Share This
Na Mwandishi wetu

MIONGONI mwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na hili la kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na fursa zinazopatikana katika miradi ya kimkakati na uwekezaji “Local Content”.

Hapo awali miradi mikubwa ya kimkakati na uwekezaji ilitajwa kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa Taifa lakini hata hivyo manufaa yake kwa wananchi wa kawaida yalionekana kuwa madogo au yasiyoonekana moja kwa moja.

Hivi sasa kuna jitihada za makusudi ya Serikali ambapo dhana ya ushirikishwaji kikamilifu kwa Watanzania katika miradi ya kimkakati inatekelezwa na kuleta matokeo chanya yanayoonekana kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Ushirikishwaji huu wa Watanzania unapewa vipaumbele vya uwekezaji, zabuni, fursa za ajira,uhuishaji wa teknolojia na manunuzi ya umma ili kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja na miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwenye Taifa lao.

Mikataba mbalimbali ya sekta imeainisha kwa uwazi shughuli za kushirikisha Watanzania ili kuwezesha ushiriki wa nguvu kazi za ndani na makampuni ya wenyeji.

Serikali pia imeendelea kutoa miongozo mbalimbali inayolenga kufanikisha utekelezaji wa hatua za kuongeza ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji.

Mwaka 2025, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) lilipewa jukumu la kisheria kupitia mabadiliko madogo ya Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Sura 386), ikiwemo kuratibu, kufuatilia, kutathmini na kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati na uwekezaji.

Hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi ni wa kweli, unaotoa manufaa ya moja kwa moja na unaleta tija kwa sekta zote.

Utekelezaji wa sera hizi unahimiza Watanzania kukuza ujuzi na uwezo wa ndani, kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya umma na kuhakikisha fursa za kiuchumi hazibaki mikononi mwa wachache tu.
























No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad