JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Wakulima Songwe ‘Walia’ Makato Huduma za Kibenki, Waitaja ‘NBC Shambani’ kama Suluhisho

Share This
DC, Wakulima Waomba Tawi Jipya la NBC Mlowo

Songwe, Aprili 29, 2026 — Wakulima wa Mkoa wa Songwe wametaja gharama za uendeshaji wa akaunti na kufungwa kwa akaunti zisizotumika kuwa ni moja ya sababu kuu zilizodhoofisha imani yao kwa taasisi za kifedha huku wakitaja ujio wa akaunti ya NBC Shambani isiyo na makato ya uendeshaji kama ‘mwarobaini’ wa changamoto hiyo.

Wakizungumza kwa niaba ya wakulima wenzao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika mji wa Mlowo, wilayani Mbozi, baadhi ya wakulima hao akiwemo Bw. George Mwashilanga, Bw. Nickson Dirisha na Bw. Hifadhi Anderson Mdono, walieleza kuwa changamoto hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima kushiriki kikamilifu katika mfumo rasmi wa kifedha.

“Kwa muda mrefu wakulima wengi wamekuwa wakikatishwa tamaa na makato ya mara kwa mara ya uendeshaji wa akaunti pamoja na hatari ya kufungwa kwa akaunti pindi zisipotumika.’’

“Hali hii imeathiri kwa kiasi kikubwa imani ya wakulima kwa huduma rasmi za kibenki kwa kuwa mbali na makato wamekuwa wakipata usumbufu wa kwa mara kufufua upya akaunti zao kutokana na ukweli kwamba kipato cha mkulima ni cha msimu’’ alisema Bw Mwashilanga

Hata hivyo, wakulima hao waliipongeza akaunti ya NBC Shambani, wakieleza kuwa ni suluhisho linaloendana na uhalisia wa mahitaji yao. Walibainisha kuwa kutokuwepo kwa makato ya uendeshaji na urahisi wa usimamizi wa akaunti, hususan kutozuiliwa kirahisi, ni hatua muhimu ya kurejesha imani na kuhamasisha ujumuishwaji wa kifedha.

“Bidhaa hii imegusa moja kwa moja changamoto zetu kama wakulima. Kutokuwepo kwa makato na uwepo wa unafuu katika usimamizi wa akaunti kunatupa fursa ya kurejea na kuamini mfumo rasmi wa kifedha,” alisema Bw. Dirisha, akiongeza kuwa wako tayari kuwa mabalozi wa kuhamasisha wakulima wengine kujiunga na huduma hiyo.

Hafla hiyo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega, na iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika (AMCOS) pamoja na washiriki wa mnyororo wa thamani wa kilimo. Pia walikuwepo maofisa wa NBC wakiongozwa na Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Bw. Abel Kaseko.

Katika hotuba yake, Bw. Mbega alitambua changamoto zilizobainishwa na wakulima na kuipongeza NBC kwa kuja na suluhisho linalolenga moja kwa moja mahitaji yao. Alisisitiza umuhimu wa huduma za kifedha zilizo rafiki na nafuu katika kukuza sekta ya kilimo, ambayo inachangia takribani asilimia 80 ya mapato ya Wilaya ya Mbozi.

“Ni muhimu kushughulikia changamoto hizi za kimuundo ili kujenga upya imani kati ya wakulima na taasisi za kifedha. Mipango kama NBC Shambani inaleta si tu huduma za kifedha, bali pia inakuza nidhamu ya fedha na ustahimilivu kwa wakulima,” alisema.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa NBC kupanua huduma zake kwa kufungua tawi katika mji wa Mlowo, akibainisha kuwa kwa sasa wakulima wengi hulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo katika miji ya Tunduma na Mbeya.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Bw. Kaseko, alisema kampeni hiyo ya miezi minne inalenga kuhamasisha wakulima wa mazao ya kimkakati kama kahawa na ufuta kutumia huduma rasmi za kifedha. Aliongeza kuwa wakulima watakaoshiriki wana nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato.

“Sekta ya kilimo inaajiri takribani asilimia 65 ya Watanzania. Dhamira yetu ni kuendelea kubuni suluhisho jumuishi na bunifu zinazokidhi mahitaji halisi ya wakulima. NBC Shambani ni hatua muhimu katika kufanikisha azma hiyo,” alieleza.

Uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani Songwe unaashiria juhudi mpya za kuziba pengo kati ya wakulima na huduma rasmi za kifedha, huku wadau wakionesha matumaini kuwa kushughulikiwa kwa changamoto hizo kutachochea ushiriki mpana zaidi, kuongeza uzalishaji na kuleta ukuaji endelevu katika sekta ya kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega (katikati), akijipongeza sambamba na maofisa waandamizi wa benki ya NBC baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC, yenye lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo ufuta na kahawa mkoani Songwe. Hafla hiyo ilifanyika jana kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wakulima. Wengine pichani ni Meneja wa NBC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi. Zubeider Haroun (kulia), Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Bw. Abel Kaseko (wa pili kulia), Meneja wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Bi. Dorothea Mabonye (wa pili kushoto) na Meneja wa NBC Tawi la Tunduma Bw Shedrack Mpanda.


Katika hotuba yake, Bw. Mbega (pichani) alitambua changamoto zilizobainishwa na wakulima na kuipongeza NBC kwa kuja na suluhisho linalolenga moja kwa moja mahitaji yao. Alisisitiza umuhimu wa huduma za kifedha zilizo rafiki na nafuu katika kukuza sekta ya kilimo, ambayo inachangia takribani asilimia 80 ya mapato ya Wilaya ya Mbozi.

Meneja wa NBC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi. Zubeider Haroun (pichani) akizungumza kwenye hafla hiyo

Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Bw. Abel Kaseko (kulia) pamoja na Meneja Mahusiano Idara ya Kilimo Benki ya NBC Bi Vivian Sakoe (kushoto) wakifafanua kwa wakulima mkoani Songwe kuhusu zawadi mbalimbali pamoja na mikopo inayotolewa na benki ya NBC kupitia kampeni ya Wekeza na NBC Shambani Ushinde.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega, akifurahia sambamba na wakulima pamoja na maofisa wa NBC wakati wa hafla hiyo.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi, maofisa mbalimbali wa NBC walipata wasaa wa kufafanua kwa wakulima kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo mahusisi kwa wakulima ikiwemo mikopo ya pembejeo na zana za kilimo, bima za afya na kilimo pamoja na kutoa elimu kuhusu nidhamu ya fedha.

Katika hafla hiyo wakulima walipata wasaa wa kusikiliza na kutoa mrejesho kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo.

Hafla hiyo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega, na iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika (AMCOS) pamoja na washiriki wa mnyororo wa thamani wa kilimo. Pia walikuwepo maofisa wa NBC wakiongozwa na Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Bw. Abel Kaseko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad